Je simu za mkononi zinasababisha kansa ya ubongo? Utafiti mpya waja na majibu

0
Sambaza

Moja ya swali ambalo watumiaji wengi wa simu za mkononi huwa wanauliza; Je simu za mkononi zinasababisha kansa ya ubongo?

Kansa ya ubongo – kiswahili cha shule, saratani ya ubongo ni moja ya hofu kubwa ambaye imekuwa ikihusishwa na utumiaji sana wa simu za mkononi.

Je simu za mkononi zinasababisha kansa ya ubongo

Je simu za mkononi zinasababisha kansa ya ubongo? Utafiti mpya waja na majibu

Tafiti kadhaa zimefanyika ila kuna tafiti mpya iliyofanyika kwa undani zaidi imeleta matokeo yake.

Tafiti hii mpya imeitishwa na kusimamiwa na shirika la Marekani linalojihusisha na usalama wa vitu na vyakula kwa watumiaji – FDA (Food and Drug Administration) kwa kushirikiana na kitengo kinachodili na masuala yahusuyo sumu (National Toxicology Program).

SOMA PIA:  WhatsApp: Desemba 31 2017 ndio mwisho kwa simu janja hizi kufanya kazi!

Utafiti umechukua miaka miwili.

Simu kuweza kuwasiliana na mtandao wa mawasiliano kuna miyonzi ambayo inakuwa inachia – ‘radiofrequency radiation’, miyonzi hii haina ukali mkubwa kama miyonzi inayotolewa na vipimo vya X-ray ambavyo vinatoa miyonzi inayotambulika kama ‘ionizing radiation’. Miyonzi ya ‘ionizing radiation’ inaweza sababisha uharibu wa DNA kwenye mwili unaoweza sababisha saratani (kansa).

Nini kilifanyika?

Kwenye utafiti huo kundi la panya liliwekwa kwenye mazingira yaliyozungukwa na miyonzi ya radiofrequency muda wote. Na kiwango cha miyonzi hiyo kiliwekwa juu kuzidi hali ya kawaida ya miyonzi inayotolewa na simu tunazozitumia.

Moja ya matokeo ya ripoti hiyo yalionesha panya wa kiume ndio waliathirika zaidi, walipata uvimbe flani ulioanza kukua maeneo ya mioyo yao. Panya wa kike waliokuwa kwenye eneo hilo hilo hawakupata. Hila hakuna ata panya mmoja alioonekana kupata aina yeyote ya saratani (kansa).

SOMA PIA:  Kongamano la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) kufanyika Oktoba 26 na 27, Dar Es Salaam

Pia cha ajabu kilichotokea ni kwamba kwa wastani kundi la panya lililokuwa kwenye mionzi ndio liliishi muda mrefu zaidi kuliko ambalo lipo eneo la bila miyonzi. Hii wanasema itakuwa imetokea tuu.

Panya hao waliwekwa kwenye eneo dogo lililowekwa kiwango cha juu cha mionzi ya radiofrequency katika mfumo wa 2G na 3G. Wameishi kwenye eneo hilo kwa muda wa miaka miwili. Pia kulikuwa na kundi jingine lililokuwa limewekwa bila kupata mionzi.

SOMA PIA:  Nokia matatani kwa wizi wa teknolojia!

Kwa makidirio umri wa miaka miwili wa panya ni takribani miaka 70 ya mwanadamu.

Matokeo ya hadi sasa ya utafiti huu yasihusishwe moja kwa moja na madhara yanayoweza tokea kwa utumiaji wa simu wa wanadamu – kwa sababu panya hawa waliwekwa kwenye kiwango cha juu sana cha miyonzi kuliko kiwango cha kawaida kinachotolewa na simu. – Walisema watafiti hao

Watafiti hao wamesema wanaendelea na uchunguzi na pia wataruhusu watafiti wa nje kusoma data hizo kwa ajili ya kuhakiki matokeo ya tafiti hii.

Vyanzo: TheVerge na tovuti mbalimbali

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com