Je, unajua kuwa Mkono ‘huathiri’ mawimbi ya simu? #Utafiti

0
Sambaza

Inaweza kuwa jambo la kushangaza lakini imebainika kuwa mikono yetu huathiri mawimbi ya simu. Je, ni mkono upi ambao ni sahihi kushikilia simu yako? TeknoKona imeipata hii na ipo tayari kukujuza.

Utafiti umebaini kwamba mkono unaathiri jinsi simu yako inapokea mawimbi. Utafiti huo unasema simu tofauti hufanya vizuri ikiwa imeshikiliwa kwa kutumia mkono mmoja kuliko mkono mwingine. Simu ambazo zilifanyiwa utafiti zilikuwa: Apple iPhone 6, Samsung Galaxy S7 and S7 Edge; Sony Xperia Z3 na Z5 na nyinginezo zikiwa LG G5; Huawei P9, Nexus 6P na 5X.

SOMA PIA:  Rasmi: Uzinduzi wa iPhone 8 kufanyika Septemba 12 mwaka huu

Prof. Gert Pedersen, kutoka chuo kikuu cha Aalborg anasema kwamba antena (kifaa kinachopokea mawimbi) za simu huwa zimewekwa mahali ambapo binadamu hushikilia simu yake, na hivyo kuathiri jinsi simu inavyopokea mawimbi.

Mikono yetu huathiri mawimbi (signals) tunapofanya mawasiliano.

Mikono yetu huathiri mawimbi (signals) tunapofanya mawasiliano.

Simu ambazo huathirika zikishiliwa kwa mkono wa kushoto

Miongoni mwa simu zinazofanya vyema zikiwa zimishikiliwa kwa mkono wa kushoto:

  • Samsang Galaxy s7 Edge
  • Microsoft Lumia 650
  • Huawei P9

Simu janja ambazo mawimbi yake huathirika zikishikwa kwa mkono wa kulia

Miongoni mwa simu zinazofanya vyema zikiwa zimishikiliwa kwa mkono wa kulia:

  • iPhone 6S Plus
  • LG G5
  • HTC 10
SOMA PIA:  Ripoti: Biashara ya mtandaoni yaongezeka kwa wananchi wa Kenya

iPhone 6s Plus kutoka Apple zilionyesha kuwa mawimbi ya simu hupatikana vyema kwa asilimia 300 iwapo zikishikwa kwa mkono wa kulia kuliko mkono wa kushoto.

Ukitaka simu yako aina ya iPhone 6s plus kupata mawimbi vizuri pale unapiga simu, ishikilie kwa mkono wa kulia.

Ukitaka simu yako aina ya iPhone 6s plus kupata mawimbi vizuri pale unapiga simu, ishikilie kwa mkono wa kulia.

Utafiti wa kitaalamu ambao unasema ukitumia simu yako bila kuishika kunaimarisha upatikanaji wa mawimbi ikilinganishwa na wakati ambapo umeishikilia.

Kutokana na kwamba simu janja nyingi zimefanyiwa utafiti; ni muhimu kwa maelezo ya simu kuhusu ni mkono upi ni mzuri kushikilia ili kuweza kupata mawimbi mazuri wakati wa kufanya mawasiliano kuwekwa wazi wakati wa kununua simu husika.

Vyanzo: BBC, Express

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com