Jiandallae 3: Simu Janja mpya kutoka Korea Kaskazini

0
Sambaza

Unapoitaja nchi ya Korea Kaskazini wazo la kwanza linalomjia mtu ni ubora wao wa utengezaji wa makombora hatari ya kivita pamoja na silaha za nyuklia.

Ni kweli, Korea kaskazini inaaminika kumiliki zaidi ya silaha 1000 zenye uwezo tofauti ikiwemo kombora la maasafa marefu ambalo linaweza kuishambulia Marekani.

Lakini si tu Korea Kaskazini ni wataalamu wa silaha za kivita, hata kwenye upande mwingine wa teknolojia zingine wapo vizuri. Na moja ni utengenezaji wa Simu janja.
Kampuni moja ya Korea Kaskazini imetoa simu janja iliyozalishwa ndani ya nchi hiyo yenye muonekano kama wa Iphone.

SOMA PIA:  Ijue Simu mpya ya mkunjo yenye vioo viwili ya Samsung Galaxy W2018

Simu hiyo itajulikana kwa jina la Jiandallae 3 imeripotiwa kutengenezwa na Mangyongdae Information Technology Corporation ya nchini humo.

airtel tanzania bando

Picha zilizotolewa  zinaonesha simu hiyo ikiwa katika muonekano wa kupendeza na kuvutia. Simu hiyo inaonesha imetengenezwa kikamilifu kwa lugha ya kikorea.

Hata hivyo hakuna habari iliyotolewa juu ya simu hiyo, isipokuwa jina lake, muonekano wa Skrini yake inayoonesha maua ya kikorea na baadhi ya programu zilizopo.

Taarifa zinasema simu hiyo ilizinduliwa mwezi machi mwaka huu lakini picha zake zimeoneshwa mwishoni mwa wiki.

SOMA PIA:  WileyFox: Kampuni ya simu inayotaka kunufaika na uamuzi wa Uingereza kutoka EU

Programu mbalimbali zinaripotiwa kupatikana katika simu hiyo ikiwemo Kikokoteo cha hesabu (Calculator), Mchezo wa karata wa Kikorea, progaramu ya picha (Photo App) na Kivinjari cha wavuti.

Korea Kaskazini imekuwa ikitoa idadi ya simu za mkononi katika miaka kadhaa iliyopita katika kukabiliana na uhitaji wa wananchi wao. Bidhaa nyingi kutoka nje ya nchi haziruhusiwi.

Korea Kaskazini imekuwa ikitumia vitu vingi vya kwake yenyewe bila kutegemea vya nchi za nje. Hata mfumo endeshi wa Kompyuta wanatumia wa kwao unaojulikana kama Red.

SOMA PIA:  Simu ndogo unayoweza 'Kuizungushazungusha'

Taarifa nyingi kutoka Korea Kaskazini zimekuwa zenye usiri sana, Teknokona tutakuwa nawe katika kukahabarisha taarifa zote kuhusu ujio wa simu hiyo mpya ya Jiandallae 3.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com