Kampuni ya simu ya Tigo imeanzisha huduma inayoitwa JIHUDUMIE ambayo itamsaidia mteja aliyetuma muamala wa fedha kimakosa kuweza kurejesha fedha zake kwa njia rahisi na haraka zaidi.
Huduma hiyo imetambulishwa julai 12 na kutangazwa na Mtendaji mkuu kitengo cha Tigo Pesa, Hussein Sayed kwa wanahabari kwa kusema huduma hiyo itamuwezesha mteja kuzuia miamala yoyote ya kutuma fedha ikiwa atagundua kuwa amekosea.
Mteja akikosea kutuma pesa hahitaji msaada wa moja kwa moja kutoka kitengo cha huduma kwa wateja bali atapiga menyu ya Tigo pesa (*150*01#) kisha atachagua huduma ya Jihudumie na kufuata maelekezo yatakayojitokeza kuwezesha kurudisha muamala wake.
Huduma hii haitatumiwa kwa wale ambao pesa imeshatumwa kimakosa na mpokeaji ameshaitoa hapo anatakiwa kufanya mawasiliano na kitengo cha huduma kwa wateja.