Jinsi Gani Ya Kutumia Mfumo wa BitTorrent! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Jinsi Gani Ya Kutumia Mfumo wa BitTorrent!

3
Sambaza

Najua ushawahi kujiuliza ni jinsi gani utaweza kushusha /’download’ vitu mbalimbali kama nyimbo, tamthilia flani unazofuatilia na unapata shida kuziona, makala flani (documentary), au ata filamu flani, vitu ambavyo vanaweza kuchukua muda mrefu kuvi’download kwa kawaida.

Tena ukiangalia suala la mwendo (speed) mdogo wa intaneti hili linakuwa kikwazo,  kwani unaweza ukaanza alafu intaneti ikasuambua wakati hata unakaribia kumaliza. Hapa ndo umuhimu wa kutumia mfumo wa ‘torrent’ katika kushusha mafaili makubwa kwa madogo unakuja.

Mfumo huu ni wa umoja katika kushusha kitu, yaani ukianza kushusha faili flani utakuwa unashusha kutoka kwa watu wengi yaani hata maelfu. Fikiria hivi, unandoo na unachota maji, kwa mfumo wa kawaida utakuwa unachota moja kutoka kwenye bomba moja, ila kwa mfumo wa torrent ni sawa na kuchota maji kutoka mabomba mengi kwa wakati mmoja. Hii inasaidia kuongeza mwendo wa intaneti katika kushusha, na faida nyingine ni kwamba ata kama intaneti au umeme utakatika ghafla usihofu kwani baadaye ukija kuwasha faili lijajiendeleza kujishusha pale lilipoishia mara ya mwisho.

Je jinsi gani ya Kutumia?

INAYOHUSIANA  Ifanye akaunti yako ya YouTube ikuingizie pesa

1.  Shusha programu ya BitTorrent:

Programu za BitTorrent ndo zitakazokusaidia katika kushusha badala ya Kivinjari( au ‘Browser’ kwa Kiingereza) kama Firefox, Google Chrome na zingine.
Programu maarafu za BitTorrent ni pamoja na BitLord, BitComet, Vuze, BiTtornado, µTorrent, BitTorrent pamoja na QBitTorrent (Unaweza ukabofya kwenye hayo majina na kwenda kushusha). Nashauri Vuze, uTorrent, BitTorrent au QBittorrent.

2. Tambua Sheria

Wengi hudhani kila kitu ni bure kwenye intaneti, ila si hivyo. Kitu pekee kinachotulinda kwa kiasi flani ni kwamba kwenye nchi nyingi zinazoendelea kama Tanzania hakuna sheria na kama zipo hazina nguvu sana katika masuala ya haki miliki kwenye intaneti. Kwa hiyo kazi ni kwako!

3. Jifunze Misamiati

Haya maneno ni ya kizungu ila ni muhimu kuyajua kwani yatakusaidia kugundua kama faili hilo litashuka upesi zaidi au litachukua muda mrefu.
  • Leecher – Mtu anayelishusha(download) ilo faili kwa wakati huo.
  • Seeder – Mtu anayepakia(uploading) faili hilo kwa wakati huo.  ‘Seeders’ wakiwa wengi, ndio ‘Leechers’ au watu wanaoshusha wataweza kulishusha kwa mwendo mkali zaidi(high speed download).
  • Tracker – Sio muhimu sana, ila ni taarifa inayolihusu ‘torrent’ file hilo na usaidia kupata taarifa juu ya Leechers na Seeders la hilo faili kutoka mitandao mbalimbali.
  • Faili la Torrent (*.torrent) – Mara nyingi hili ni faili dogo, ukishalishusha huwa linaipa programu yako ya BitTorrent kuhusu wakina nani wanahilo faili (kama filamu, muziki, n.k) ili BitTorrent iweze kulishusha kutoka kwao.
INAYOHUSIANA  Intagram yaenda mbali, sasa inawatumiaji hai bilioni moja

 4. Tafuta Mafaili ya Torrent

Kwa kuanzia unaweza kwenda www.kat.ph kwa  vitu mbalimbali kama filamu, muziki, tamthilia, programu n.k

5. Fungua hilo Faili la Torrent Ulilolishusha kutoka Mitandao Hiyo.

Ukilibofya mara mbili (double click) au kulifungua kwa namna nyingine yeyote litafunguliwa na programu ya BitTorrent uliyokwenye kompyuta yako. Inaweza kukuuliza unataka ku’save’ wapi faili hilo litakaloshushwa chagua sehemu na acha programu ifanye kazi yake.
NB: Kumbuka faili lenye ‘Seeders’ wengi na ‘Leechers’ wachache litashusha haraka zaidi.

6. Likimaliza kushusha kazi kwako…..

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

3 Comments

Leave A Reply