Jinsi ya ku-convert Mafaili Yoyote kwenda Mfumo wa PDF kwenye simu za Android

0

Upo na simu janja yako tuu na una document, picha, n.k unazotakiwa kuzituma katika mfumo wa PDF, iwe kupitia barua pepe n.k. Leo nitakuonesha apps muhimu zinazokusaidia kutengeneza mafaili ya PDF kwenye simu yako ya Android.

Ku’scan karatasi ulizonazo kutengeneza mafaili ya PDF

Mfano una risiti, au karatasi ambayo unataka kuhifadhi au kutuma kwa mtu kutumia simu yako na document hiyo kuwa kwenye mfumo wa PDF. App ya CamScanner itakusaidia kwa urahisi kutengeneza PDF mpya kutokana na mafaili uliyonayo.

Convert faili mfumo wa pdf

App hii ni bure na inapatikana katika soko la apps la Google Play.

Unaitumiaje?

Kupitia app hiyo utaweza kupiga picha mafaili yako na picha hizo zitahifadhiwa katika mfumo wa PDF moja kwa moja. Baada ya hapo utaweza kutuma kwa njia ya barua pepe, kuifadhi kwenye simu au ata kwenye huduma za DropBox na Google Drive.

Pia utaweza ata kuchukua picha ulizonazo tayari kwenye simu yako (Gallery) na kuzi-convert kwenda mfumo wa PDF

Ku’convert Meseji, Barua pepe, ukurasa na mtandao n.k

Katika eneo hili app inayofahamika kwa jina la PDF Converter:Documents to PDF ndio ipo vizuri zaidi. Kupitia app hii utaweza ku’convert’ barua pepe, meseji, namba za simu na kurasa za mitandao kwenda moja kwa moja kwenye mfumo wa mafaili ya PDF.

convert faili mfumo wa pdf

App hii inapatikana bure katika soko la Google Play

Kuitumia

kupitia app hiyo utaona kwa urahisi wapi pa kufanya nini kupitia utambulisho mwepesi baada ya kufungua app hiyo.

Download/Pakua kutoka Google Play – CamScanner PDF Converter:Documents To PDF

Hizo ndio app mbili zinazoweza kukusaidia kuhamishia karibia aina zote za mafaili kwenda PDF, je unafahamu app nyingine? Tuambie na shauri wengine kupitia eneo la comment.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com