Jinsi Ya Ku Log Out Facebook Kwa Simu iliyopotea! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Jinsi Ya Ku Log Out Facebook Kwa Simu iliyopotea!

0
Sambaza

Kama umepatwa na majanga haya ya kuibiwa kifaa chako inaweza kuwa simu au hata kompyuta yako, pole. Lakini kama hayajakufika kumbuka yanaweza kukukuta, hivyo basi ni vyema kujua nini utafanya kama yakitokea.

Wengi wakipoteza au kuibiwa vifaa vyao hukimbilia kubadili neno siri (password) za mitandao yao ya kijamii hasa facebook, lakini kwa nini ufanye hayo yote wakati kuna njia rahisi kabisa?.  Mtandao wa kijamii wa Facebook unaweza tumiwa vibaya na mtu ambae amepata simu yako pasopo na kibali (ameiba) na kukuweka katika matatizo.

Haitajalisha ulikua unatumia simu gani kama ni Android, Windows, iPhone basi unaweza Log out Facebook kwa kutumia njia hii ifuatayo.

INAYOHUSIANA  Ukuaji wa teknolojia katika kamera za kwenye simu

enter site MUHIMU: Njia hii inaweza fanyika kwa kutumia kompyuta tuu na sio simu. Kama hutaki meseji,picha na mambo yako mengine muhimu Facebook kuonwa na mtu mwingine ambae ana simu yako basi futa yafuatayo

  • Kwa kutumia kompyuta ingia katika akaunti yako ya Facebook
  • Click kwenye Menyu ya kushuka na kisha chagua ‘Settings’facebook teknokona2
mobile-settings-min

Kipengele Cha ‘Mobile’ Katika Settings

log-out-facebook-min

Log Out Katika Simu Iliyopotea/Ibwa

Sio ngumu sana eeeh? Hongera kwa kufanya hivyo. Lakini pia Teknokona inakushauri uondoe namba yako ya simu uliojiandikishia facebook maana itakua imejishikiza katika ile simu uliyoibwa/poteza.

INAYOHUSIANA  Apple kufanyia matengenezo bidhaa zao bure

Jinsi Ya Kufanya Hivyo

  • Rudi katika upande wa ‘Mobile‘ katika Settings
  • click Remove mbele ya namba ya simu ili kuitoa facebook. Hii itaongeza ulinzi katika simu yako iliyoibwa.

Sasa akaunti yako ya Facebook iko salama, na wewe ndio umefanikisha hilo. Haijalishi unatumia simu ya aina gani kwani njia ya kufanya zoezi hili ni moja. Tuandikie mawazo yako kama unaona njia hii ina msaada kwako. Dondosha lako la moyoni sehemu ya comment hapo chini.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Leave A Reply