Jinsi Ya Kubadilisha Akaunti Yako Ya Facebook Kuwa Page!

2

Sambaza

Kama inavyojulikana Facebook ni moja kati ya mitandao ya kijamii ambayo inatikisa dunia kwa sasa. Licha ya hivyo pia Facebook

wana vipengele vingi sana na bado wanaendelea kutoa vingine vingi ambavyo vinaifanya Facebook izidi kuwa Juu. Hivi Ulisikia Hii: Facebook Waja Na Hello – App Mpya Kwa Simu Za Android

Achana na hiyo je ushawahi sikia kuwa unaweza badilisha akaunti yako ya facebook na kuwa page? yaani  watu wataanza kuku ‘Like’ baadala ya kuku ‘Add As A Friend’. Najua unaweza ukawa na maswali mawili hapo juu ya kwanini na ni kwa vipi?.. Ngoja nikujibu Yote

Kwa Nini Ubadilishe Akaunti Yako Ya Facebook Kuwa Page

Kama unatumia ukurasa wako wa facebook kufanya biashara za mtu au hata kutangaza biashara ya mtu si sahihi ni unakiuka vigezo na masharti. Biashara zote inabidi zifanyike katika ‘Page’ na sio akaunti za kawaida kama unazotumia. Kwa kifupi huruhusiwi kutumia ukurasa wako wa facebook kuwasilisha kitu kingine chochote kisichokuwa kinahusiana na wewe kwa mfano biashara yako.

INAYOHUSIANA  WhatsApp na machapisho ya picha za mnato

Kutokana na hayo basii unahitaji Page ili utangaze na kuendesha biashara yako. Sasa si vizuri kuanza na moja kabisa. Si unaweza tuu kubadilisha akaunti yako ikawa ndio page yako. Hii itakurahisishia kwa sababu hata watu waliokuwa marafiki zako watakua ndio watu wako wa kwanza kwanza kulike page hiyo

Pia kumbuka Facebook inaruhusu akaunti ya kawaida kumiliki marafiki 5000 tuu lakini ukiwa na page hata kufikisha bilioni inawezekana. Sasa baada ya kujua sababu twende tukajua tutafanikisha vipi jambo hili.

Jinsi Ya Kubadilisha Ukurasa Wako Wa Facebook Kuwa Page

Kabla ya kuchukua maamuzi ya kuendelea ni vyema kujua taarifa gani zitahama kutoka katika ukurasa wako na kwenda samabamba katika Page yako. — Hapa utajua nini kitabaki na nini kitapotea —

INAYOHUSIANA  Machapisho ya picha na video kuweza kuweka muziki

Nini Kitahama

– Kama nilivyosema awali marafiki zako wote na followers wako watakuwa ndio watu wanao ‘ like’ page yako

– Username Yako ndio itakuwa username ya Page Yako

– Picha ya kwenye profile lako ndio itakua picha ya kwenye Page yako

– Bado utakuwa na mamlaka sawa katika Page zingine ambazo unaziendesha

Nini Hakitohama/Kitafutika

Post zako, Picha na Album zote hazitakuwa zimehama bali zitafutika hivyo Teknokona inashauri uhifadhi taarifa zako zote kabla ya kufanya zoezi hili

Pia utapoteza cheo chako katika makundi yote ambayo yapo chini yako. Hivi tunashauri kuwa kabla ya kufanya zoezi hili uchague mtu na umeweke awe ndio mwendeshaji wa makundi hayo.

INAYOHUSIANA  Programu tumishi ya Facebook yazidi kutoswa

Sasa unaweza kuendelea na kubadilisha akaunti yako ya Facebook kuwa Page kwa kufuata Maelekezo haya.

  • Log in katika ukurasa wako wa facebook
  • Fuata Link Hii Kuanza kubadilisha Akaunti yako kuwa Page
  • Chagua Aina ya page unayotaka katika machaguo yaliyojitokeza

Convert-Profile-to-Page-Facebook

  • katika kuchagua aina ya page chagua pia ‘Category’ inayokufaa kisha bofya ‘Get Started’

Select-Specific-Category

Safii sasa umefanikiwa kubadilisha Akaunti yako ya facebook kuwa page. Ni matumaini yetu kuwa tatizo lolote au ukikwama katika kipengele chochote juu ya makala hii utatuandikia swali lako. Pia usisahau kudondosha comment yako muhimu hapo chini.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

2 Comments

  1. sesalla mohd masimba on

    Nahitahi tofauti baina ya page na akaunti ya kawaida.na pia nahitaji kujua ili fungue page unarakiwa uwe na marafiki wangapi?

Leave A Reply