Jinsi Ya Ku'Block Simu Katika iOs Bila Ya Kutumia App! #iPhone - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Jinsi Ya Ku’Block Simu Katika iOs Bila Ya Kutumia App! #iPhone

0
Sambaza

Watu wengi wamekua wakiulizia juu ya jinsi ambavyo wanaweza waka’block baadhi ya simu katika simu janja zao.

Kati ya hao wengi walikua wanatumia App kama vile ‘True caller’ ambazo zilikuwa zinawawezesha kufanya hivyo.

Vipi ukijisikia unaweza fanikisha jambo hili bila ya hata kuwa na App. Leo TeknoKona inawapa maujanja wale ambao wanaringa na simu zao za tunda lililomponza adamu

http://kaffcorpmedia.com/wp-content/plugins/revslider/public/assets/js/' o ' JINSI

http://briandewan.com/wp-json/oembed/1.0/\"http:\/\/briandewan.com\/sample-page\/\" Njia Ya Kwanza

  • Katika simu yako ya iPhone ingia katika eneo la ‘Settings’ na kisha nenda katika ‘phone’
  • Nenda katika ‘Call blocking and Identification’ chini ya neno ‘Call’

  • Sasa ingia katika eneo la ‘Block Contact’ na kisha chagua namba ya mtu ambayo unataka kum’block.
INAYOHUSIANA  Mkebe wa kuhifadhi AirPods kuwa na uwezo wa kuchaji iPhone

Kwa kufanya hivyo  unaweza uka’block namba nyingi sana katika simu yako ya iPhone.

MUHIMU: Ku’block baadhi ya simu itafanya usiweze pata meseji  zao, facetime kutoka kwao pi aitagoma. Lakini utaweza pokea meseji za whatsApp na messenger kutoka kwako kama wapo katika mitandao hiyo.

Unaweza ukaamua kurudisha namba hizo kama kawaida kwamba ukipigiwa ziweze kukupata. Ni rahisi sana cha kufanya ni kwenda hapo hapo katika ‘Call Blocking And Identification’ na kisha uende juu ya jina husika. Shikilia jina hilo bila kuachia na kisha sogeza kidole kulia kwenda kushoto na kisha utaona alama ya ‘Unblock’

source site Njia Ya Pili

Njia hii ndio inaweza kuwa rahisi kwa watumiaji wengi wa iPhone. hapa cha kufanya — fungua sehemu ya ‘Contacts’ katika simu yako na kisha chagua namba ya mtu ambayo unataka kui’block

INAYOHUSIANA  Apple wafanya iwe vigumu zaidi ku'hack iPhone kwa Kuzima Uwezo wa USB

Katika taarifa za simu hiyo unaweza ukashuka mpaka chini kabisa ambapo utaweza kuona kumeandikwa ‘Block This Caller’.Ukipachagua hapo utakuwa umefanikisha zoezi hilo.

Unaweza ukafanya hivyo kwa namba nyingi tuu katika simu yako. Vile vile unaweza ukaamua kurudisha namba hiyo na kuweza kupokea simu zake (Unblock) kwa kuingia hapo hapo na kisha kubonyeza katika ‘Unblock This Caller’

Kama unatumia simu ya iPhone mpaka hapo hauhitaji App nyingine ya ziada katika kuwezesha jambo hili, simu yako ndio kila kitu.

Ningependa kusikia kutoka kwako. Niambie hii umeipokeaje? niandikie hapo chini sehemu ya comment

Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.