Kwa siku zinatumwa na kupokelewa barua pepe (E-mail) zaidi ya bilioni 205 kupitia mtandao wa Gmail. Namba hii kubwa ya barua pepe inapatikana kwa kuwa watu wamejiandikisha batika vitu mbalimbali kama vile mitandao tofauti tofauti kwa kutumia barua pepe (Gmail) zao.
Kutokana na kuwa watu wanpokea barua pepe nyingi sana kwa siku, inakua ni vigumu sana kuzisoma zote na hata pia kuzipangilia. Saa zingine inawabidi kufuta barua pepe nyingi walizopokea kwa mkupuo, na pia inaweza tokea zile zenye umuhimu na zenyewe zikafutwa bila kusudio.Hili kama likikutokea leo Teknokona inakupa ufumbuzi.
MUDA WA KUFUFUA
Kwanza kabisa jambo la muhimu kujua ni kwamba barua pepe zote zilizofutwa huwa zinakaa katika folda linasloitwa ‘Trash‘. Maisha ya barua pepe katika folda hilo ni siku 30 (mwezi) tuu. Baada ya hapo barua pepe hiyo itafutika moja kwa moja.Na baada ya hapo hautakuwa tena na uwezo wa kuweza kuifufua barua pepe hiyo.
NJIA ZA KUFUFUA BARUA PEPE
- Fungua akaunti ya Gmail kwa kutumia kompyuta
- Ikishafunguka nenda katika kibox cha ku ‘search’ pale juu na kisha andika “in:trash” kisha bofya Enter.
- Fungua barua pepe ambayo unataka kuifufua
- ‘Click‘ katika sehemu ya ‘Move To‘ na kisha chagua ‘Inbox‘
Mara tuu ukishamaliza fanya hivyo moja kwa moja barua pepe yako inatolea katika ‘trash‘ na kwenda moja kwa moja katika folda la ‘Inbox’
USHAURI KUTOKA TeknoKona.
TeknoKona inakushauri wewe mtumaji na mpokeaji wa barua pepe (hasa katika Gmail) kuwa badala ya kufuta (delete) barua pepe zako inabidi uziweke katika sehemu ya kumbukumbu (Archive) . Kama una barua pepe ambayo ni ya umuhimu basi haina budi kufanya hivyo kwa kumbuka endapo ukifuta barua pepe hiyo baada ya siku 30 itafutika moja kwa moja.
JINSI YA KUWEKA BARUA PEPE KATIKA ARCHIVE
- Fungua akaunti ya Gmail
- Fungua barua pepe unayotaka kuiweka katika kumbukumbu (Archive)
- Angalia alama ya ‘Archive‘ na kisha ui ‘click‘ kama inavyoonyeshwa kwenye picha hapo chini
- Baada ya hapo barua pepe yako itahifadhiwa.
No Comment! Be the first one.