Jinsi Ya Kufuta Akaunti Ya Facebook Moja Kwa Moja! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Jinsi Ya Kufuta Akaunti Ya Facebook Moja Kwa Moja!

1
Sambaza

Kama umechoka tumia mtandao wa kijamii wa facebook au hata kama unataka kubadilisha ukurasa huo huna budi kuufuta. Achana na kusitisha kwa mda (Deactivate), nazungumzia kuufuta kabisa katika mtandao wa facebook.

Hii inamaanisha baada ya kufuta ukurasa huo hakuna mtu yeyote anaeweza kuuona na hiyo ina maana hata wewe huwezi kuuona tena. wengi wetu njia hii hatuifahamu, sisi tunajua tuu ile ya ku ‘deactivate’ ambayo tunafanyaga na baada ya muda tukijisikia kurudi facebook, tunaweza fanya hivyo kwa ku ‘log in’ tena katika akaunti zetu

Leo TeknoKona inakufundisha maujanja (Mapya kwako) kuhusu jinsi ambavyo unaweza kufuta akaunti yako ya facebook kwa muda na jinsi ambavyo unaweza futa moja kwa moja

see url JINSI YA KUSITISHA KWA MUDA (DEACTIVATE)

INAYOHUSIANA  Mechi za La Liga kuonyeshwa bure na Facebook

Ngoja kwanza tuangalie namna ya kusitisha akaunti zetu za facebook kwa muda ili kama tukitaka tuendelee kuzitumia tuweze fanya hivyo pia.Zifuatazo ni njia za kuwezesha hivyo:

  • Fungua akaunti yako ya facebook
  • Click katika menu (ile ya kuanguka chini iliyopo juu upande wa kulia)
  • Baada ya hapo ‘click’ Settings

Facebook Menu

deactivate

JINSI YA KUIPATA AKAUNTI ULIYOISITISHA KWA MDA (DEACTIVATE)

Hii ni raahisi kabisa —wewe unahisi itakua ni vipi? haha!— hapa hakuhitaji jasho kabisa. Ingia facebook alafu ‘log in’ kwa kutumia taarifa zako ulizokuwa unazitumia kama kawaida. Moja kwa moja itafunguka akaunti yako. Endelea kufurahia kutumia facebook

INAYOHUSIANA  Punguza kupokea maombi ya urafiki Facebook

JINSI YA KUFUTA AKAUNTI YA FACEBOOK MOJA KWA MOJA

Kama umeamua kuwa hutaweza endelea tumia akaunti yako ya facebook au mitandao ya kijamii imekuchosha (ndio! mitandao inaweza ikakuchosha saa zingine). Ikitokea hivyo unaweza kuwaza kufuta ukurasa wako moja kwa moja sio? Njia hii haijulikani kwa watu wengi lakini asante kwa TeknoKona na wewe utakuwa fundi ndani ya mda mchache

Kabla ya yote inashauriwa mtu kushusha (download) nakala ya taarifa zako za facebook

Kufanya Hivyo, Fuata Njia Hizi

  • Fungua akaunti yako ya facebook
  • Click katika menu (ile ya kuanguka chini iliyopo juu upande wa kulia)
  • Kisha ‘click’ katika settiings
  • Katika “General” chagua “Download a copy of your Facebook data.” kwa ku’click’ hapo

download-a-copy-min

INAYOHUSIANA  Facebook yapoteza wateja kutokana na GDPR

delete-min

Baada ya hapo utakuwa umefuta akaunti yako ya facebook moja kwa moja. Hii inamaanisha kuwa hutaweza kuitumia akaunti hiyo kamwe maana hii ni tofauti na kusitisha kwa mda (deactivate)

Facebook inachukua mpaka siku 90 kufuta mambo yote katika mtandao wa kijamii wa Facebook. Kuna baadhi ya taarifa haziwezi futika kwa mfano meseji ambazo umewatumia marafiki. Bado zitabakia katika eneo lao la kusoma meseji.

Tuambiae kama wewe ni mmoja kati ya wale wanaotaka kufuta akaunti zao za Facebook moja kwa moja na ulikua hujui njia za kufuata kufuta akaunti ya Facebook. TeknoKonaDotCom ndio mtandao wako namba moja katika masuala yote ya teknolojia.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

1 Comment

  1. Pingback: Jinsi ya kufuta kabisa akaunti ya Twitter #Maujanja - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Leave A Reply