fbpx

Jinsi ya kufuta kabisa akaunti ya Twitter #Maujanja

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +

Sambaza

Inawezekana kabisa umetokea kuuchukia kabisa mtandao wa kijamii wa Twitter kutokana na sababu mbalimbali lakini hujui jinsi gani ya kuondoa akaunti yako na basi roho yako iwe na amani.

Twitter ni moja ya mitandao ya kijamii ambayo kwa asilimia kubwa ina watumiaji wachache mataifa mengi duniani (Tanzania ikiwemo). Lakni si kwamba Twitter ni mtandao mbaya ila kwa wale wanapenda kuandika vitu virefu (barua 😆 😆 ) lazima wauchukie mtandao wa kijamii wa Twitter kutokana na uchache wa herufi ambao unaruhusiwa kwa tweet moja.

Unapoamua kuondoa/kufuta akaunti yako ya Twitter maana yake ni kwamba utakuwa huwezi tena kufuatikia tena habari za wale ambao ‘umewafuata’ kwenye Twitter mathalani sisi TeknoKona na hivyo kushindwa kupata habari zetu kupitia Twitter na za wengine wote ambao umewafuata kwenye Twitter.

Unaweza pia ukaamua ‘kuifunga kwa muda’ (deactivate) akaunti yako kwa muda na pale na baada ya muda fulani (chini ya siku 30) ukaweza kuitumia tena. Kujua tofauti kati ya kufuta kabisa na kufunga kwa muda BOFYA HAPA!.

INAYOHUSIANA  Simu imepotea tuma IMEI kwenda cop@vsl.net - Hii habari ni ya uongo, usifanye hivyo

Hatua za kufuata ili kuweza kufuta akaunti ya Twitter.

Ili kufuta akaunti yako ya Twitter kitu cha kwaza ni kusitisha kwa muda akaunti hiyo na kama utakuwa hujaitumia akaunti hiyo ndani ya siku 30 baada ya kuisitisha kwa muda Twitter wataanza mchakato wa kuifuta kabisa akaunti hiyo, mchakato unaweza kuchukua wiki nzima 🙄 🙄 . Fuata hatua zifuatazo ili kuweza kusitisha akaunti yako kwa muda:-

 • Ingia kwenye akaunti yako ya Twitter kwa kupitia kwenye kivinjari (Firefox, Chrome, n.k) kwani hawezekani kusitisha akaunti ya Twitter kupitia programu tumishi.
 • Ingia Settings inayopatikana baada ya kubofya kwenye picha yako upande wa kulia pembezoni kabisa.

  Kwenye Settings ndio mwanzo kabisa wa mchakato mzima wa kusitisha akaunti ya Twitter.

 • Kisha bofya neno ‘Deactivate my account’ utakaloliona mwisho kabisa kwenye ukurasa wa Settings.

  Bofya kwenye neno ‘Deactivate my account’ ili kwenda ukurasa unaofuata na kuendelea na hatua nyingine.

 • Ukiridhika na maelezo ambayo yapo chini ya kipengele cha ‘Deactivate my account’ bofya ‘Deactivate [username unayotumia kwenye Twitter]’ kukubali. Mathalani @teknokona. 

  Maelezo ya kina kuhusiana na mchakato mzima wa kusitisha akaunti ya Twitter.

 • Kisha weka nywila yako unayotumia kwenye mtandao wa Twitter kuruhusu kusitisha akaunti yako ya Twitter.

  Weka nywila ili kuridhia kusitisha akaunti yako ya Twitter.

Baada ya kufuata hatua hizo utakuwa umeweza kusitisha akaunti yako ya Twitter na hatimae mchakato wa kuifuta kabisa kuanza kuifuta kuanza baada ya siku 30. Ukibadilisha mawazo na kutaka kuitumia tena akaunti yako ya Twitter unaweza kufanya hivyo ndani ya siku 30 tangu siku ulipoisitisha.

Chanzo: Telegraph

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.