Jinsi ya kufuta kabisa akaunti ya WhatsApp

0
Sambaza

Je, umeamua kuifuta kabisa akaunti yako ya WhatsApp? Kama jibu ni ndio basi leo tutakuelekeza namna ya kufanya hatua kwa hatua kufanikisha azma yako.

Kwa kuwa katika makala kadhaa za huko nyuma tulielekeza namna ya kufuta akaunti za Facebook, Twitter, n.k basi na leo tumeona hilo pia tulielekeze kwa akaunti za WhatsApp.

Wengi wamekuwa hawafuti akaunti zao za WhatsApp bali huacha kutumia kwa kubadili namba za simu na kufungua akaunti nyingine ilihali ile ya kwanza bado ikionekana ipo ingawa haitumiki tena.

Kabla ya kuingia hatua hizo lazima ufahamu kwamba hakuna kitakachorudi pindi utakapoamua kuirudisha tena akaunti yako ya WhatsApp. Ni kwamba ukifanikisha zoezi hili hutaweza kurudisha tena ujumbe wowote uliowahi kutumiwa au kutuma. Pia utakuwa umejitoa rasmi katika makundi yote ya WhatsApp.

SOMA PIA:  Namna ya kuhamishia App katika Memori kadi! #Maujanja

Namna ya Kufuta kabisa akaunti ya WhatsApp.

Ili kufuta akaunti ya WhatsApp ni lazima kufuata hatua zifuatazo bila kuruka hata hatua moja:-

1. Fungua WhatsApp katika simu yako. Ingia katika Setting (Angalia dot tatu upande wa kulia juu),

Jinsi ya kufuta kabisa akaunti ya WhatsApp

Jinsi ya kufuta akaunti ya WhatsApp: Hatua ya kwanza.

2. Ingia kwenye akaunti (Account),

Jinsi ya kufuta akaunti ya WhatsApp: Hatua ya pili.

3. Chagua Delete my account,

Jinsi ya kufuta akaunti ya WhatsApp: Hatua ya tatu.

4. Ingiza namba yako ya WhatsApp halafu bonyeza kwenye kitufe cha Delete my account,

Jinsi ya kufuta akaunti ya WhatsApp: Hatua ya nne.

5. WhatsApp itakuuliza kwanini unafuta akaunti yako. Chagua sababu moja ya
kufuta akaunti yako,

Jinsi ya kufuta akaunti ya WhatsApp: Hatua ya tano.

6. Kubali kufuta akaunti yako na baada ya hapo utaona mrejesho kuwa umefanikiwa kufuta akaunti yako ya WhatsApp.

Jinsi ya kufuta akaunti ya WhatsApp: Hatua ya sita.

Uthibitisho kuwa akaunti ya WhatsApp imefutwa.

Tunaamini umeelimika vya kutosha kupitia makala hii, kama una maoni au swali usisite kutuandikia hapo chini kwenye sehemu ya kutoa maoni nasi tutakujibu kwa haraka kadri iwezekanavyo.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com