Jinsi Ya Kugeuza (Chini Juu) Maneno Unayoandika Katika Mitandao Ya Kijamii Na Kwingine!

0
Sambaza

Hivi katika pita pita zako katika mitandao ya kijamii haujawahi kukutana na maneno ambayo yamegeuka yaani yanaonekana kama yamepinduka hivi (chini juu).

Kama ulishawahi na hujua namna ya kufanya au hujawahi basi hapa uko sehemu sahihi. Kwa kutaka sifa kabisa ngoja nkusalimie kwanza, ¡¡ɐuoʞouʞǝ┴ nqᴉɹɐʞ ¿oʞɐ⅄ ᴉɹɐqɐH

Haya ngoja niache sifa, kwa kifupi ni kwamba kuna njia nyingi ambazo unaweza kuzitumia kuweza kufanya zoezi hili ila kwa leo ntakuaonyesha hii moja tuu ingawa kuna mitandao mingi inaweza ikawezesha zoezi hili

SOMA PIA:  MASTODON:Ufahamu mtandao mbadala wa Twitter unaokuja kwa kasi

1. Upsidedowntext

2. Manytools.org

3. Fliptext.net

Kwa kutumia njia ya kwanza ya Upsidedowntext.com ni kwamba unaweza ukageuza maneno yakawa chini juu katika simu za Android, iOs , Windows na hata katika kompyuta yako.

Mtandao Wa UpSideDownText

Kwa kutumia kifaa chako ingia katika mtandao wa www.Upsidedowntext.com/ na ukifanikiwa utaona vimetokea viboksi viwili

Kile cha juu utaweza kuandika neno ambalo unataka lionekane chini juu, neno hilo litaonekana chini juu katika kiboksi kingine cha pale chini.

SOMA PIA:  Namna ya kuwa WhatsApp Tester (Tumia toleo la beta) #Maujanja

Baada ya neno kutokea pale chini likiwa limeshageuka chini juu basi unaweza ukalinakili (copy) na kisha ukaenda kuli’paste’ katika mtandao wa kijamii.

Neno Ukiwa Unali'Paste Katika Mtandao Wa Kijamii

Neno Ukiwa Unali’Paste Katika Mtandao Wa Kijamii (WhatsApp)

Najua ukitumia njia hii unaweza ukapa maswali mengi sana, watu wanaweza wakakuuliza kuwa umewezaje kufanya hivyo. Kitu kizuri ni kutokuwa mchoyo waambie TeknoKona wamekujuza.

Muonekano Wa Maneno Yaligeuka (Chini Juu) Kwa Watumiaji Wa iOs

Muonekano Wa Maneno Yaligeuka (Chini Juu) Kwa Watumiaji Wa iOs

Sambaza maujanja haya na kwa marafiki zako pia ili mfutahie wote. Ningependa kusikia kutoka kwako, hii umeipokeaje? niandikie hapo chini sehemu ya comment. Tembelea TeknoKona kila siku ili kupata habari na maujanja mbali mbali ya teknolojia.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com