Jinsi ya Kuhifadhi Namba za simu katika Mtandao – #Android #Maujanja

0
Sambaza

Makala hii itakusaidia kuweza kuelewa jinsi ya kuhifadhi namba za simu zilizo katika simu yako kwenye mtandao ili uweze kuzipata hata utakapopoteza simu yako.

Kila mtu angependa pindi anapopoteza ama anapobadilisha simu aweze kuendelea kuwa na namba za simu alizokuwanazo katika simu yake ya zamani lakini sio wote wanaojua jinsi ya kufanya hili, makala hii itakufundisha hatua kwa hatua.

Zipo njia mbali mbali ambazo zitaweza kukusaidia kuweza kupata contacts zako zilizokua katika simu yako ya zamani leo tutaziangalia njia mbili ambazo ni maarufu zaidi. Njia ya kwanza ni ile ya kuhakikisha kwamba majina yako yote katika simu yako yanahifadhiwa katika akaunti yako ya Google ambayo unaitumia katika simu yako ya android, na njia ya pili ambayo ni rahisi zaidi ni ile ya kutumia App ambazo zipo kwaajiri ya kuhifadhi contacts katika mtandao.

> Njia ya kwanza: Kuhifadhi kumbukumbu katika akaunti yako ya Google.

Njia ya kwanza ni kuhakikisha kwamba  namba za simu (contacts) zote katika simu yako  zimehifadhiwa katika akaunti yako ya Google, hii utaweza kwa kuhakikisha kila namba ya simu unayo ihifadhi katika simu yako basi unaihifadhi katka akaunti ya Google.

Njia hii ndiyo tunayokushauri utumie…

> Jinsi ya kuhifadhi? 

Kila unapohifadhi namba ya simu katika simu yako basi utaulizwa je unataka kuhifadhi  katika sim card yako, katika memory ya simu ama katika akaunti ya google? hivyo basi unatakiwa kusema  kuwa unataka kuhifadhi  katika akaunti ya Google na si namna nyingine yeyote ile. Jambo jingine ambalo unatakiwa kuhakikisha ni kwamba simu yako kila wakati inafanya synchronization hii husaidia zile kumbukumbu zako za kwenye simu kuweza kuhifadhiwa katika mtandao.

Namba ya simu hapa itaweza kuwa backed up

Namba ya simu iki hifadhiwa katika akaunti ya Google

Namna ya kuzipata namba zako za simu katika simu nyingine!

Pindi utakaponunua ama kubadilisha simu basi utakapoingiza tu barua pepe yako (mara nyingi unapoanzisha simu mpya utaombwa kuingiza anuani yako ya barua pepe) basi hapo hapo kumbu kumbu zako zitakuwa zimeletwa na kuwekwa katika simu yako mpya.

SOMA PIA:  Airplane Mode ni nini? Fahamu matumizi na faida zake!

Angalizo!

Kama una namba za simu katika simu yako ambazo tayari ulisha zihifadhi katika kumbukumbu ya simu ama katika kumbukumbu ya simu kadi yako basi hizi namba hautaziona hadi pale utakapo zihifadhi tena katika kumbukumbu ya akaunti ya Google.

Njia ya pili ni kuhifadhi kumbukumbu katika App.

Zipo application nyingi sana tofauti tofauti ambazo moja ya kazi yake ni kuhakikisha kwamba kila namba ya simu iliyopo katika simu yako inahifadhiwa sehemu fulani katika mtandao, kwa namna hii utaweza kuzipata hizi namba zako za simu wakati wowote na katika kifaa chochote ili mradi tu umeiweka hii application katika kifaa chako kipya.

> Namna ya kuhifadhi Namba zako kwa njia hii!

Shusha app kwa ajiri ya kufanya kazi hii zipo nyingi katika Google play lakini mimi nakushauri uitumie Netquin ambayo hata mimi naitumia na naiamini lakini unaweza kutumia yeyote utakayo ipenda, baada ya kudownload basi tengeneza akaunti katika app hii (unaweza kutengeneza akaunti kwa kutumia taarifa zako za facebook kwa haraka zaidi).

Namba huifadhiwa hapa

Sehemu iliyoandikwa Cloud back up ndiyo sehemu inayotumika kuhifadhi contacts

Baada ya hapo unachotakiwa kufanya ni kuanza ku upload namba zako za simu kwa kwenda katika sehemu iliyoandikwa cloud backup kama inavyoonekana hapo juu na utakapoingia uta backu up contacts

SOMA PIA:  Fahamu jinsi ya kutuma GIF's kwenye WhatsApp

> Namna ya kuzipata namba zako za simu katika simu nyingine!

Utakapo kuwa katika simu nyingine ama kifaa kingine unachotakiwa kufanya ni ku shusha app uliyokua unatumia katika simu ya zamani, kisha utaingina katika akaunti yako kwenye app hiyo na kisha utakwenda katika sehemu yaku restore contacts na utazishusha contact zako zote ambazo ulikuwa umezi upload kipindi cha nyuma.

namba

Jinsi ya ku back up na ku restore contacts katika App

Angalizo!

Utahitaji kuwa unafanya backup ya contact kila ambapo umeongeza contacts mpya katika simu ili kuhakikisha kuwa hupotezi namba za simu mpya maana kama namba ya simu hukuwa umeiupload basi simu ikipotea nayo itakuwa imepotea.

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTube, Telegram na Google Plus

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com