Jinsi ya Kuikatalia WhatsApp kutuma data zako kwenda Facebook

0
Sambaza

Hivi karibuni tuliandika kuhusu WhatsApp kutuma data za watumiaji wake kwenda mtandao wa Facebook.

Soma Pia – WhatsApp kutuma data kuhusu utumiaji wako kwenda Facebook

Kama sehemu ya kutokwenda nje ya sheria WhatsApp wanakupa uwezo wa kukataa suala hilo ndani ya siku 30.

airtel tanzania bando

Inakuwaje?

Kama bado haujapata ombi la kukubali mkataba (Terms and Privacy Policy) mpya kutoka WhatsApp basi unaweza pata muda wowote.

Ingawa hakuna eneo la kukataa makubaliano hayo ila kuna kanjia karefu ambacho WhatsApp wanajua wengi hawatafuata ili kuwawezesha kukataa utoaji wa taarifa zao za utumiaji wa WhatsApp kwenda Facebook.

Hatua za kufuata

Hapa chini ni muonekano wa mkataba huo wa Terms and Privacy Policy unavyoonekana pale unapokujia kwenye app ya WhatsApp.

Kuikatalia WhatsApp

Kuikatalia WhatsApp

Usibofye eneo la kukubali ‘AGREE’, bali bofya eneo la chini la  “Read more about the key updates to our Terms and Privacy Policy.” , ukibofya hapo maelezo zaidi yatafunguka na pia kuna eneo utaliona lishapigwa vyema (tick) likiruhusu WhatsApp kutuma data zako kwenda Facebook. Ondoa tiki (vema) halo na kisha kubali.

Kama ulishakosea na kukubali mkataba huu bila ya kuondoa hili basi unaweza kusahihisha kwa kutembelea eneo la settings – Account Menu, baada ya hapo ondoa ‘vyema’ kwenye enero la Share my account info.

Soma Pia – WhatsApp kutuma data kuhusu utumiaji wako kwenda Facebook

SOMA PIA:  USB OTG ni nini? Je simu yako ina #teknolojia hii? - Fahamu

Vipi je wewe una mtazamo gani na mabadiliko haya yaliyoletwa na WhatsApp? Je unaona ni sawa kuwapatia data zako ili wazitumie kwa ajili ya kuboresha matangazo yao hasa hasa katika mtandao wa Facebook?

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. – Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom

| mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com