Jinsi ya Kuiwezesha Kompyuta Kujizima Yenyewe Usiku

Jinsi ya Kuiwezesha Kompyuta Kujizima Yenyewe Usiku

1
Sambaza

Je, wewe ni mmoja wa wale wanaotumia kompyuta hadi usiku wa manane na huwa unasinzia na kusahau kuzima? Au huwa unatakaga kusikiliza mziki wa taratiiiibu ukiwa unautafuta usingizi? Wengi wetu tunafahamu kuhacha kompyuta usiku kucha kunachosha kompyuta yako au betri ya laptop yako na saa nyingine ata uniti za umeme wako 🙂

Leo TeknoKona tutakufundisha jinsi ya kuweka mipangilio (setting) flani kuiwezesha kompyuta kujizima pale muda flani utakapofika au ata pale tuu ambapo itakuwa haitumiki.

Kufanikisha jambo hili itabidi uifahamu programu iitwayo ‘Task Scheduler’!

buy finasteride walgreens 1. Fungua programu ya Task Scheduler!

Unaweza ipata enter kwa kubofya ‘Start’ kisha tafuta kwa kuandika ‘Task Scheduler’ au kwa Windows 7 bofya ‘Start’ → ‘Control Panel’ → ‘System and Security’ → ‘Administrative Tools’ → ‘Task Scheduler’. Na kama unatumia toleo la Windows 8, basi bofya Win key, kisha andika “schedule tasks”, na bofya kuchagua “Schedule tasks” katika matokeo.

INAYOHUSIANA  TTCL na vifurushi vya usiku

2. Bofya ‘Create Basic Task’

kompyuta-kujizima-wikihow

buy Mysoline from canada Bofya ‘Create Basic Task’, kisha andika taarifa zozote muhimu za kukufanya ukumbuke pale utakapoondoa au kutaka kufanya mabadiliko siku flani. Asaasa jaza sehemu ya jina – ‘name’, kwenye maelezo sio muhimu. Kisha ‘BOFYA NEXT’

3. Eneo la Task Trigger, Chagua ni mara ngapi kompyuta ifanye hivi,

…………….unaweza chagua kama ni kila siku, au mara moja kwa wiki, n.k

kompyuta-kujizima-wikihow2

Kwa kuwa tunataka iwe kila siku basi chagua ‘Daily’ kisha bofya ‘NEXT’. Hapa utaona sehemu za kuweka muda unaotaka kompyuta iwe inajizima, sehemu ya ‘Recur every X Days’ yenye maana ya hali hiyo ijirudie kila baada ya siku X, acha iwe 1 (Moja), kisha ‘BOFYA NEXT’

INAYOHUSIANA  Windows 98 yatimiza miaka 20 tangu kuzinduliwa kwake

4. Katika eneo litakalofuata baada ya kubofya ‘NEXT’, chagua ‘Start a Program’

kompyuta-kujizima-wikihow3

Kisha bofya ‘NEXT’

5. Andika eneo lilipo programu inayotakiwa kufanya kazi.

Kiuhalisia kompyuta inapozimika kuna programu ya ndani kabisa inayofanya kazi hiyo, basi kwenye eneo la “Program/script” andika, C:WindowsSystem32shutdown.exe au unaweza kukopi na ku’paste’ moja kwa moja kama tuliivyoandika hivyo

kompyuta-kujizima-wikihow4

Eneo la “Arguments” andika /s

Bofya ‘NEXT’

6. Kwenye eneo la mwisho angalia kama kila kitu kipo sahihi

…..vile unavyotaka kiwe, unaweza badilisha jina tena la kumbukumbu.

kompyuta-kujizima-wikihow5

Kama umeridhika na kila kitu basi bofya ‘Finish’

Tayari! Sasa tegemea kila siku katika muda ule uliouchagua kompyuta yako itakuwa inajizima yenyewe.

INAYOHUSIANA  Microsoft na WhatsApp waunganisha nguvu kufanya kitu

Kumbuka kama utataka kufanya mabadiliko au kuanza upya kabisa na kuondoa chaguo basi fungua tena programu ya Task Scheduler kisha bofya ‘Task Scheduler Library’, moja ya chaguo litakalokuwa linaonekana upande wa kushoto.  Ukibofya utaona jina kama ulivyolichagua katika vitu vilioorodheshwa, basi utaweza kufuta au kubofya na kufanya mabadiliko.

Kumbuka unaweza ungana nasi pia kupitia akaunti zetu zaTwitter, Facebook Na Instagram

 *Picha – www.wikihow.com

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

1 Comment

  1. Pingback: Leawo Music Recorder: Rekodi muziki na sauti kwenye Kompyuta

Leave A Reply