Jinsi Ya Kujua Muda Uliotumia Kwa Kila App (#Android & #iOS)! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Jinsi Ya Kujua Muda Uliotumia Kwa Kila App (#Android & #iOS)!

0
Sambaza

Kutokana na teknolojia ilivyokua na jinsi ulimwengu wa mitandao ya kijamii ulivyotuteka, tumekuwa tukitumia simu zetu mara kwa mara. Je unajua ni muda gani unatumia kwa kila App?

where to buy antabuse in canada

http://synergyohio.org/portfolio/synergy-conference-2014/ Ni vyema kujua jambo hili kwani litakusaidia hata wakati unajifanyia tathimini juu ya App za muhimu kwako na zile ambazo hazina umuhumu.

Hii ni kwa wote watumiaji wa Android na wale wa iOS. Njia ni kama zifuatazo.

Kwa Android.

  • Ingia katika Google Play Store na kisha tafuta QualityTime au ingia hapa
  • Pakua App na kisha ifungue.. Itakubidi uingie katika App hii kwa kutumia akaunti ya Facebook (kama huna nenda katika ‘Create account’)
INAYOHUSIANA  Piga simu kwa watu wengi kwa njia ya WhatsApp

  • App itakuuliza maswali kadhaa kama utaweza yajibu ni sawa tuu lakini unaweza uka’skip’
  • Utambuliso mfupi utakuwepo kwa ajili yako
  • Baada ya hapo ingia katika ‘Let’s Start’ na kisha ‘Permit’

  • Kisha utakuwa umefanikisha hilo. Baada ya muda ukirudi katika App hii utaanza kuona muda ambao umeutumia ukiwa katika Apps mbali mbali.

http://ceec.ca/wp-json/oembed/1.0/embed?url=http://ceec.ca/ Kwa iOS.

Huku hakuhitaji kuwa na App mbadala ili kulijua hili.

  • Ingia katika ‘Settings’ kisha nenda kwenye ‘Battery’

Jinsi Ya Kuangalia Muda Uliotumia Katika Apps Katika iOS

  • Subiri kwa muda kidogo ili kuiwezesha simu zako ikusanye taarifa ya kila App.  Baada ya hapo ingia katika kialama cha saa ili kuona muda wa matumizi kwa App mbalimbali
INAYOHUSIANA  Facebook ina mbinu ya kuwa karibu na mkufunzi

Mpaka hapo umeona ni muda gani unatumia kwa kila App Vile vile cha muhimu ni kwamba umeona ni App gani ambazo huwa zinakula muda wako mwingi. Soma Pia Jinsi Ya Kuzuia Uraibu (Addiction) Wa Simu Janja Kila Mara!

Hii inaweza ikakusaidia katika kuhakikisha kuwa unajizuia katika kutumia baadhi ya App ili uokoe muda wako kwa kufanya mambo mengine.

Ningependa kusikia kutoka kwako, Niandikie hapo chini sehemu ya comment, Je unuona hii itakusaidia?

Kumbuka Kutembelea TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.