Jinsi Ya Ku’Log Out’ Instagram Kwa Kutumia Kifaa Kingine!

0
Sambaza

Ni mara ngapi huwa tunaomba tungekuwa na uwezso wa ku’sign out’ katika akaunti zetu katika vifaa vingine. Hii haijalishi kama utakua umeibiwa kifaa chako au utakua na sababu zako binafsi.

Ukiachana na Gmail na Facebook ambao wao wanatoa njia rahisi ya kulog out kwa kifaa kingine, Instagram kidogo iko tofauti. Hapa itakubidi mpaka ubadilishe neno siri kwa kutumia akaunti nyingine.

Kuna sababu tofauti tofauti lakini unaweza ukawa pia uwesahau akaunti yako katika simu ya rafiki yako njia hii itakusaidia.

SOMA PIA:  StoreDotFlashBattery: Betri inayojaa chaji chini ya dakika moja! #Teknolojia

JINSI

  • Fungua App ya Instagram katika kifaa (Simu) kingine na kisha log in.
  • Nenda katika ‘Profile’ na kisha bonyeza vidoti vitatu.

Eneo La Vidoti Vitatu Katika Profile

  • Shuka chini mpaka uone ‘Change Password’  na kisha ingia hapo.

Eneo La ‘Change Paassword’

  • Kama kawaida jaza hapo kwa kuingiza nenisiri la zamani na kisha ingiza jipya na kisha lirudie.

Namna Ya Kubadilisha NenoSiri

Ukifanikiwa kufanya hivyo hapo utakuwa umeweza Ku’log out’ kwa katika vifaa vingine vyote ambavyo bado vilikua na akaunti yako. Ni rahisi sana sio?….

SOMA PIA:  HP kulipwa takribani trilioni 6.6 za Tsh na Oracle baada ya kushinda kesi

Kwa Kutumia PC itakubidi ufuate hatua hizi hizi na kisha uende kubadilisha nenosiri lako.

Mpaka hapo naona utakuwa umeshava juu ya hili, ningependa kusikia kutoka kwako. Niandikie hapo chini sehemu ya comment

Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com