Jinsi Ya Kuongeza Spidi Ya WiFi Ya Nyumbani! #Maujanja - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Jinsi Ya Kuongeza Spidi Ya WiFi Ya Nyumbani! #Maujanja

0
Sambaza

Pale vifaa vyetu vinavyokuwa vimeishiwa na bando (MB/GB) WiFi huwa ndio kimbilio letu. WiFi hii ndio hutuwezesha kufanya mambo mbalimbali katika vifaa vyetu kwa kutumia huduma ya intaneti

Kuna wengine WiFi wanazo majumbani kwao, wanazitumia kwa matumizi madogo madogo ya kifamilia, wengine zipo katika maofi. Na zingine zipo tuu mitaani.

Jinsi Ya Kuongeza Spidi Ya WiFi
WiFi hizi unaweza ukashangaa zinatumiwa na watu wengi sana mara moja na kwa pamoja. Hii inaweza ikazisababisha zikawa na spidi ndogo.

can you buy Levetiracetam in mexico Je ni mambo gani unaweza kufanya ili kufanya Spidi ya intaneti ya WiFi ikaongezeka?

http://vmustard.com/vsa-recovery/?share=facebook 1. Weka Router (Inayosambaza WiFi) katika Eneo Sahihi

Router zote inabidi zisifichwe kamwe, inabidi ziwekwe kwenye eneo la uwazi ambapo hakuna vitu ambavyo kwa namna moja au nyinigne vitasababisha network isiwe nzuri kama vile ukuta n.k

Jinsi Ya Kuongeza Spidi Ya WiFi

Mfano Wa WiFi Router

Ili kuwa na uhakika kabisa ‘Router’ hiyo inabidi ikae katika eneo la uwazi kabisa na ikiwezekana ikae kati kati ya nyumba ili kuwezesha kila mtu kuweza kupata network kwa urahisi

INAYOHUSIANA  VPN ni nini? Fahamu app 3 za bure za Huduma ya VPN

can you buy diflucan over the counter in ireland 2. Zuia Muingiliano Wa Ki ‘Network’
Vifaa kama vile vile vya kuangalia watoto wanafanya nini (baby Monitors), simu na hata majiko ya umeme ya uokaji (microwave ovens) vinaweza vikasababisha WiFi yako ikawa inazingua katika swala zima la network. Kuondoa ile Router na kuipeleka mbali kidogo na vifaa hivyo inaweza ikasaidia pia

Jinsi Ya Kuongeza Spidi Ya WiFi

Baadhi Ya Vifaa Ambavyo Vinaingilia Katika Swala Zima La Network

3. Imarisha Ulinzi
Unaweza ukashangaa tuu intaneti ya WiFi yako imekua finyu tuu lakini ukichunguza vizuri unagundua kuwa sio nyie tuu (wanafamilia) mnaoitumia, bali kuna watu wengi kama vile majirani n.k. Hali hii pekee inaweza sababisha intaneti ikawa chini. Ili kuhakikisha kuwa hili halijitokezi basi huna budi kuweka ulinzi kwa kuweka vitu kama NenoSiri (Password) na vile vile usiweke wazi neno siri hili kwa watu ambao hawahusiki na WiFi hiyo

Jinsi Ya Kuongeza Spidi Ya WiFi

Weka NenoSiri Kwa Ajili Ya Ulinzi

4. Zuia Apps/Vitu Ambazo Zinakula Data Kwa Kiasi Kikubwa
Kuna vitu vinakula data sana vitu kama vile kuangalia video katika mtandao na kusikiliza muziki. Ukiachana na kuangalia mafaili ya video mbalimbali ambao yana ubora wa HD unaweza ukashangaa katika familia kuna mtu anatumia intaneti hiyo katika kushusha (Download) mafaili makubwa kabisa. Vitu kama hivyo inabidi vifanyike wakati hakuna mtu mwingine ambae anatumia WiFi hiyo na nyakati bora ni za usiku

INAYOHUSIANA  Kingo Root: Programu/App ya Kuroot Simu za Android na Windows

Kama WiFi yako ilikuwa inasuasua mpaka hapo nadhani utakua umeshaipatia dawa. Niandikie sehemu ya comment hili wewe umelipokea vipi? Ningependa kusikia kutoka kwako

Kwa habari na maujanja mbalimbali yanayo husu teknolojia tafadhali tembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kila siku. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.