Jinsi ya Kupakia WhatsApp yenye Ladha Tofauti - Teknokona

Jinsi ya Kupakia WhatsApp yenye Ladha Tofauti kwenye Simu yako

0
Sambaza

WhatsApp tofauti zinaongeza vionjo vya WhatsApp ya kawaida kwenye simu yako. Unaweza kupata muonekano mzuri zaidi, meseji za kitofauti, kuamua mambo mengi zaidi ya utumiaji na kwa ujumla, kupata ladha tofauti kabisa ya WhatsApp.

http://novelfineries.com/product/demekin/ Soma hapa kufahamu aina hizi tofauti za WhatsApp na ubora wake – Aina 3 Tofauti za WhatsApp

Kupata ladha tofauti za WhatsApp, unaweza kufanya yafuatayo:

Android:

http://pncwinterfest.com/special-events/special-events-calendar/ 1. Shusha WhatsApp mbadala hapa:
WhatsApp Plus
OGWhatsApp
2. Okoa Meseji zako:

Ni muhimu kufanya ‘back-up’ ya meseji zako. Ingawa WhatsApp inafanya hivi mara kwa mara, ni muhimu kufanya hivi mwenyewe. Ukifanya hivi, utaokoa meseji zako zisipotee unapoweka WhatsApp mpya au hata unapobadili simu.
Kuokoa meseji fanya hivi: Menu-> Settings -> Chat Settings -> Backup conversations.
Subiri kinachoendelea kwenye skrini kiishe.

INAYOHUSIANA  iPhone X yadumu kwa wiki mbili chini ya mto

3. Toa WhatsApp yako ya kawaida:
WhatsApp ya ladha tofauti haiwezi kufanya kazi sambamba na WhatsApp ya kawaida na hivyo, inafaa uitoe (uninstall) kabla ya kuipakia.
Kufanya hivi: Ingia kwenye settings za simu yako -> Application Manager -> tafuta WhatsApp -> Uninstall.

4. Pakia WhatsApp yako mpya na fuata maelekezo ya kawaida ya kuweka WhatsApp.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ninafuatilia teknolojia kila siku na ninapenda kutoa ujuzi wangu kuhusu teknolojia. Karibu tuzungumze kuhusu teknolojia hapa teknokona!

Leave A Reply