Jinsi Ya Ku’Post Picha/Video Ktk Instagram Kwa Kutumia Kompyuta!

0
Sambaza

Pengine labda unaweza ukawa huna simu kwa kipindi hicho, tuseme imeibwa. Japokuwa tunajua kabisa ni lazima tuwe na App ya Instagram katika vifaa vyetu ndipo tuweze ku’post picha katika mtandao huo.

Lakini hapana kuna njia mbadala ambazo zinaweza zikatumika, achana na zile njia za Bluestacks au zinazofanana na hiyo. Leo TeknoKona inataka ikupe njia moja (Gramblr) ambayo kazi yake ni moja tuu.

Njia hii (Gramblr) utaweza kutuma picha yako katika akaunti yako ya Instagram tuu na hutaweza kufanya mambo mengine kama vile kuona picha za watu, ku’like au ku’comment.

SOMA PIA:  Flippy: Roboti mahususi kwa ajili ya upishi wa 'Burger'! #Teknolojia

Baada Ya Hilo Kueleweka Ngoja Nikupeleke Katika Njia Yenyewe!

1. Shusha na pakua Gramblr (inapatikana kwa Mac na Windows)

2. Ukimaliza kupakua, ifungue na kisha itakuomba uingize taarifa zako za muhimu katika akaunti yako ya Instagram (Jina/Barua Pepe, Nenosiri). Ukimaliza kujaza taarifa hizo chagua Sign Up.

Gramblr
3. Baada ya kukamilisha zoezi hilo, kuna ukurasa mwingine utafunguka. Kama unataka Ku’post video au picha chagua Apload Now.

4. Hapo una uwezo wa kuishikilia picha unayotaka na kwenda kuiachia katika kiboksi ili ijipakie au unaweza uka’click katika kicho kiboksi ili kuchagua picha.

SOMA PIA:  MASTODON:Ufahamu mtandao mbadala wa Twitter unaokuja kwa kasi

5. Baada ya hapo unaweza ukai’crop picha yako na kuchagua ‘Filters’ mbalimbali kama utataka. Kisha chagua Save na kisha Continue.

Gramblr
6. Andika ujumbe wa picha/video (Caption) na kisha Send.

Gramblr
Kingine cha kuvutia katika huduma hii ni kwamba unaweza ukaitumia kama unataka ku’post pica/video ambayo mtu mwingine ame’post (Repost). Ili kuweza kufanya hivyo itabidi utafute URL ya picha/video hiyo kicha uje kuiweka katika kiboksi kilichoko chini ya eneo la kupakia/kuweka picha/video .

SOMA PIA:  Facebook Kuja Na "Find WiFi" Kama Kipengele Kipya!

Mpaka hapo hakuna ubishi na wewe ni mtaalamu sio? Safiii, pia usisite kuniandikia lolote la moyoni au kama umekwama sehemu pia niandikie hapo chini sehemu ya comment. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com