Jinsi Ya Ku'Post Video/Picha Kutoka Katika Gallery Kwenda Katika Instagram Story! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Jinsi Ya Ku’Post Video/Picha Kutoka Katika Gallery Kwenda Katika Instagram Story!

0
Sambaza

Kwa sasa Instagram ndio mtandao wa kijamii namba moja kwa maswala ya picha na video. Mtandao huo umefanya mambo mengi sana katika kuhakikisha kuwa unajiboresha ili kuzidi kuwa namba moja.

http://essiedoessummer.com/2018/02/cocktail-blackberry-love/

enter site Moja kati ya maboresho hayo ni pamoja na kuongeza kipengele cha Stories na ‘filters’ katika mtandao huo. Japokuwa maboresho haya yanafana dhahiri na mtandao wa kijamii wa Snapchat lakini ni jambo la muhimu kwani makampuni hayo mawili yanachuana vikali.

Tatizo kubwa linakuja kuwa pale unapotaka kuchukua picha zako au video zako za kwenye ‘Gallery’ na kuzi’post kwenda katika stories za Instagram. Wengine wamepata tatizo kama hili lakini leo kama kawaida ya TeknoKona wanakupa maujanja ya kuliwezesha hilo.

INAYOHUSIANA  VIdeo za makundi kwenye Instagram sasa ni rasmi

see JINSI

  • Fungua App yako ya Instagram na kisha nenda sehemu ya ku’post ‘story’ mpya (utaliwezesha hilo kwa kuingia katika kialama cha kamera).
  • Itafunguka sehemu ambayo huwa unatumia kurekodi video mpya au kupiga picha ili ziende katika ‘stories’. Cha kufanya hapa ni ku’slide kidole juu ya skrini yako kutoka chini kwenda juu

  • Kufanya hivyo utaanza kuaona baadhi ya picha na video kutoka katika ‘Gallery’ yako. Utaweza kuchagua picha ambayo unaitaka au video na kisha kui’post.

Kwa kuipost picha/video hiyo moja kwa moja itatokea katika ‘Stories’ zako.

Mpaka hapo nafikiri na wewe utakuwa ni mtaalamu wa swala hilo. Ningependa kusikia kutoka kwako, Niandikie hapo chini sehemu ya comment. Niambie kama hili limekusaidia.

Tembelea TeknoKona Kila Siku, Kumbuka Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.