Jinsi Ya Ku’ScreenShot’ Katika Kompyuta!

0

tecno phantom 8

Sambaza

Kama zilivyo simu janja zetu tunaweza vile vile ku’screen shot’ hata ‘screen’ ya kompyuta zetu. Ni wazi kuwa kuna muda tunataka kuchukua baadhi ya taarifa fulani katika kompyuta na kunakili tukio husika katika kompyuta ikawa ndio njia rahisi kabisa

Leo TeknoKona inakuletea njia mbili za kuwezesha kulifanya hilo. pengine itategemea ni njia gani rahisi kwako ambayo utaweza kuitumia.

NJIA YA KWANZA

airtel ofa kabambe

Njia ya kwanza ambayo imezoeleka na wengi ni ile ya kubonyeza vibonyezo vya ‘FN + Prt SC’ kwa wakati mmoja. Baada ya kubonyeza vibonyezo hivyo hapo utakua umenakili chochote ambacho kilikua katika ‘Screen’ ya kompyuta yako.

Lakini hapo bado utashindwa kukiona cha kufanya basi ni kwenda juu ya picha yeyote na kisha ‘Right Click’ na kisha nenda sehemu ya Edit. Ikifungua nenda sehemu ya ‘File’ na kisha nenda katika sehemu ya ‘New”

SOMA PIA:  Namna ya kubadili folda lako kuwa la rangi uitakayo katika Windows! #Maujanja

Ukurasa mpya ukifunguka cha kufanya ni kubonyeza ‘Ctrl + V’ kwa wakati mmoja na hapo utakuwa umeweza kuiweka ile nakala yako pale

Cha mwisho kufanya hapo ni kwenda sehemu ya ‘File’ na kisha u ‘Save’ kazi hiyo katika mfumo wa picha za kawaida (GPJ). Mpaka hapo utakua umefanikisha hilo

NJIA YA PILI

Njia hii itawezeshwa kwa kutumia ‘Snipping Tool’

Kuliwezesha hili itakubidi ubonyeze alama ya ‘Windows’ katika ‘Keyboard’ ya kompyuta yako na kisha uandike neno ‘Snipping tool’, likitokea boonyeza ili kuifungua.

Ikifunguka bonyeza sehemu ya ‘New’ ili kuanza kuitumia

Bonyeza mwanzo wa eneo unalotaka kulichukua bila kuachia ‘Mouse’ shuka mpaka chini mwa eneo hilo na kisha achia ‘Mouse’  (Drag) baada ya hapo ‘Snipping Tool’ itafunguka na kuonyesha eneo ambalo umelichagua.

SOMA PIA:  Sirius A: Kompyuta ya Windows 10 inayotosha mfukoni mwako

Baada ya hapo bonyeza sehemu ya ‘File’ na kisha ‘Save’ File hilo kama picha katika eneo unalolitaka

Mpaka hapo utakua umeshafahamu njia hizi mbili. cha msingi ni kuchagua ile moja ambayo unaiweza zaidi na kisha kuanza kuitumia.

Njia Hizi Zitatumika VIzuri Kwa Watumiaji Wa Windows!

Usisahau kutembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kila siku kwa habari moto moto zinazohusu Teknolojia kwa ujumla.

Ningepeda kusikia kutoka kwako, hii umeipokeaje? Niandikie hapo chini sehemu ya comment. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com