Jinsi Ya Kushusha Video Kutoka Youtube Bila Ya Kutumia Programu Yeyote! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Jinsi Ya Kushusha Video Kutoka Youtube Bila Ya Kutumia Programu Yeyote!

0
Sambaza

Japokuwa TeknoKona imeandika makala nyingi sana ambazo zinaelezea jinsi ya kushusha video kutoka Youtube kwa kutumia Programu kama vile Tubemate, bado imekua ni gumzo kwa baadhi ya watu.

Leo tunakuletea njia rahisi sana ya kuweza kushusha video hizo. Njia hii haitahusisha utumiaji wa programu nyingine yeyote.

Kabla sijakupeleka kwenye njia hiyo cha msingi ni kwamba uhakikishe tuu kwamba intaneti yako inakasi (ili video unayoishusha isije ikafeli kabla bado haijashuka yote).

click Tuifahamu NJia Hiyo.

MUHIMU: Njia hii inakubali kwa watumiaji wa simu janja (Android tuu, simu zingine labda kujaribu) na kompyuta!.

where can i purchase colchicine HATUA 1: Fungua Video unayotaka kuishusha.

Ingia Katika Video Unayotaka Kuishusha

Mfano: Video Kutoka TeknoKona

INAYOHUSIANA  Youtube: Kipengele cha Dark Mode kwenye simu

robaxin for sale no HATUA 2: Ukurasa wa video ukishafunguka nenda katika eneo la URL naa baada ya WWW. Weka SS na kisha bofya Enter kwa watumiajia wa kompyuta na baada ya M. weka SS kwa watumiaji wa simu janja.

Weka SS Baada Ya WWW. Au M.

HATUA 3: Ukurasa mwingine utafunguka ukiwa na sehemu ya kushusha video hiyo. Kabla ya kuishusha unaweza ukachagua video hiyo iwe katika mfumo gani (mf MP4, 3GP n.k).

Chagua Aina Ya Mfumo Wa Video

HATUA 4: ukishamaliza chagua mfumo unaoutaka kisha chagua Download.

Baada Ya Kuchagua Aina Ya Mfumo Unachagua 'Download'

Baada Ya Kuchagua Aina Ya Mfumo Unachagua ‘Download’

Hongera mpaka sasa una uwezo wa kushusha video za Youtube moja kwa moja katika kifaa chako kwa mtelezo kabisa. Ningependa kusikia kutoka kwako hii imekaaje? Je kwako imekubali?.

Kwa maujanja mengine kama haya na zaidi ya haya kaa karibu na TeknoKona kila siku. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.