Jinsi ya kutumia kompyuta kupokea Simu Yoyote - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Jinsi ya kutumia kompyuta kupokea Simu Yoyote

1
Sambaza

image

Moja ya mambo ya msingi unayopaswa kujua wakati unatumia kompyuta ni kuiunga na simu yako ili isikuingilie wakati unafanya kazi au hata unapostarehe kwa kunapoangalia muvi.

Tayari njia kadhaa za kufanya hivi kwa simu za androidi na i-phone zimezungumzwa hapa Teknokona lakini kwa makala hii inazungumzia jinsi ya kutumia kompyuta yako ya Windows kupokea simu kwenye simu yoyote yenye bluetooth na kuendesha mazungumzo yako bila ya kuigusa simu.

Jambo la kwanza kufanya ni kuunga (Pair) simu yako na kompyuta kwa bluetooth. Ikiwa tayari vitumi hivyo vimeungwa, ingia kwenye mipangilio ya bluetooth ya simu yako na angalia orodha ya vifaa vilivyoungwa na simu yako.

INAYOHUSIANA  Uganda: Sheria ya kodi ya mitandao ya kijamii kupitiwa upya

Tafuta Jina la kompyuta yako, bofya mipangilio kwenye jina la kompyuta yako na angalia orodha ya huduma unazoweza kutumia na kompyuta yako.

Wezesha huduma ya ‘hands-free’. Kama utafanikiwa kuunga simu yako na pia kuiwezesha hiyo huduma basi simu ikiingia utaona upande wa kulia kushoto kidirisha kidogo kikionesha jina la mtu au namba ya anayepiga simu.

Kwa kutumia ‘earphone’ au speaker na microphone ya kompyuta yako, utaweza kuendesha mazungumzo yako. Unaweza pia kurekodi mazungumzo kiulaini.

Ukiacha bluetooth ikiwa imewaka, huna haja ya kufuata hizi hatua zilizoelezwa toka mwanzo na baadala yake itaunga moja kwa moja bila na kuonesha simu zinazoingia bila bughudha.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ninafuatilia teknolojia kila siku na ninapenda kutoa ujuzi wangu kuhusu teknolojia. Karibu tuzungumze kuhusu teknolojia hapa teknokona!

1 Comment

  1. Me kuna app flan hv nimeisahau mliiongelea kipind cha nyuma kwamba nyakat za uck ukiilengesha angan unaona kama michoro hv!

Leave A Reply