Jinsi ya kuweka Bold, tide na Italic kwenye Whatsapp - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Jinsi ya kuweka Bold, tide na Italic kwenye Whatsapp

1
Sambaza

Watu wengi husumbuka sana wanapoandika ujumbe kwenye app ya WhatsApp kutokana na hali kwamba herufi huwa na uzito sawa wa rangi katika hali ya kawaida. Mtindo huwa mmoja tuu, ila kuna namna ya kufanya kuwa tofauti.

Whatsapp: Bold, Italic na Strikethrough

order Depakote online Whatsapp: Bold, Italic na Strikethrough

http://wakethebear.org/product/wake-the-bear-hat-navy/?add-to-cart=979 Je, wajua unaweza kukoleza rangi ya herufi na kuzifanya nzito (bold), ukaziweka kwa mlazo (Italic) na pia ukaweka mstari unaozikata herufi kati (strikethrough) kwenye Whatsapp?

Unachohitaji kufanya kwanza kabisa ni kuwa na toleo la karibuni zaidi la app ya WhatsApp kwenye simu yako.

Kuweka bold

Ili kukoza rangi kwenye herufi (kufanya bold), unahitajika kutanguliza neno lako na buy Pregabalin 300 mg uk alama ya nyota na kisha kuhitimisha na alama ya hiyo hiyo ya nyota kwa mfano ukiandika *bold* itatokea ikiwa bold.

Whatsapp: Ujumbe ambao ni bolded

Whatsapp: Jinsi ya kufanya ili ujumbe wako uwe bolded  

Kuweka Italic

Ili kufanya herufi zako kuwa za mlazo (italic), unahitajika kutanguliza na mstari sakafu (underscore) na kuhitimisha na alama iyo hiyo. Kwa mfano ukiandika “_italics_” itatokea ikiwa Italics.

Jinsi ya kufanya ili ujumbe wako uwe katika mfumo wa Italics

Jinsi ya kufanya ili ujumbe wako uwe katika mfumo wa Italics

Kuweka strikethrough(tide)

Ukitaka kuweka alama ya kukata kati kwenye herufi zako, unahitajika kuanza na alama ya mawimbi  [tilde (~)] na kuhitimisha na alama iyo hiyo. Kwa mfano ukiandika “~strikethrough~” itatokea ikiwa na mstari uliokata herufi kati.

Ujumbe ukiwa katika mfumo wa strikethrough

Ujumbe ukiwa katika mfumo wa strikethrough

Kuunganisha mitindo

Unaweza ukataka kuunganisha mitindo, mfano utake  maandishi yako kuwa na bold, strikethrough na Italic kwa wakati mmoja utahitajika kutumia alama za unachohitaji katika kuanza neno lako na kuhitimisha.
Mfano, ukiandika “~_*bolditalics*_~” inafaa kutokea ikiwa bold-italics pamoja na strikethrough.

Mfano ujumbe wenye bold, italic na strikethrough

Mfano ujumbe wenye bold, italic na strikethrough

Je, umefanikiwa kuweza kufanya maandishi yawe bold, italic, strikethrough au vyote kwa pamoja?

Niandikie comment yako kama umefanikiwa au wapi hujanielewa na mimi nitakujibu. Teknokona daima tunajali wasomaji wetu.

Chanzo: BBC, WCCF Tech

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Facebook ina mbinu ya kuwa karibu na mkufunzi
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|