Kama unataka kutuma ‘post’ moja katika mitandao mingi ya kijamii itakuchukua muda kidogo kuliwezesha hilo kama hujaunganisha mitandao hiyo.
Hii ni sababu moja wapo ambayo imepelekea makampuni makubwa yanayomiliki mitandao hii ya kijamii kuja na njia kabambe ambazo zitaweza kuliwezesha hili
Lakini pengine muda mwingine sio vizuri kutuma kitu kimoja katika mitandao yote, au inaweza ukawa unataka kitu kionekana katika mtandao mmoja na kisionekane katika mwingine.
Leo TeknoKona inakuletea maujanja juu ya njia ambayo itakuwezesha kutenganisha (Unlink) akaunti ya Instagram na Facebook,
Kama Unatumia Akaunti Ya Biashara Katika Instagram
Kama unatumia akaunti ya biashara katika mtandao huo basi hutaweza kuzitengenisha akaunti hizo mbili mpaka uibadilishe ile akaunti ya biashara ndani ya instagram irudi kuwa ya kawaida.
Kufanya Hivyo Fuata Njia Hizi.
- Fungua App ya Instagram na kisha ingia katika katika ‘Profile’ lako.
- Ingia katika ‘Settings’
- Shuka chini mpaka ufikie sehemu ya ‘Switch Back To Personal Account’ kisha ingia.
- Ukishaingia hapo, unaweza badilisha na kurudisha akaunti yako katika hali yake ya kwanza (Personal account)
Kama akaunti yako sio ya biashara achana na maelezo ya hapo juu na endelea kusoma chini
Njia (Kama Unatumia Akaunti Ya Kawaida — Sio Ya Biashara — )
- ingia katika App ya Instagram na kisha nenda katika ukurasa wako (profile)
- Nenda katika Settings kwa kuingia katika alama ya settings (iphone) au vidoti vitatu (Android).
- ingia katika eneo la ‘Linked accounts’
- ingia katika eneo la ‘Facebook’ na kisha Unlink.
Baada ya hapo akaunti yako itakua imejitenga na Facebook na hutaweza kuona tena orodha ya marafiki zako wa Facebook ambao wapo katika mtandao wa Instagram.
Pia ni kwamba hutaweza ku’post’ kitu kikaenda moja kwa moja katika mtandao wa Facebook.
Mpaka hapo natumai umeweza kufanya hili, Kama lolote likitokea usisite kuuliza hapo chini sehemu ya comment.
Kumbuka Kutembelea TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.