Jinsi ya Kuzuia Video za Facebook Kujicheza Zenyewe - 'Auto Play'! #Maujanja - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Jinsi ya Kuzuia Video za Facebook Kujicheza Zenyewe – ‘Auto Play’! #Maujanja

0
Sambaza

Siku hizi Facebook wamefanya video zinazowekwa kwenye mtandao huo zianze kucheza mara moja ukiziona ata bila ya wewe kuchagua kuziangalia. Hii iwe kwenye app au kwenye mtandao, na kiukweli jambo hili linakera kwa watumiaji wengi.

Leo kupitia TeknoKona fahamu njia bora ya kufanya video za Facebook zisifanye hivyo, zi-play pale tuu unapobofya Play na si zicheze bila ruhusa na hivyo kukumalizia bando yako muhimu ya data.

Njia zitakuwa tofauti tofauti ila zinafanana kulingana na aina ya kifaa unachotumia – mtandaoni Facebook, App ya Android na kwenye app ya iOS.

video za facebook

Kama unatumia Facebook kwenye mtandao (Web)

 1. Ingia(Log in) kwenye akaunti yako ya Facebook
 2. Nenda eneo la settings za follow link video kupitia ‘ Misoprostol tablets 20 mcg no prescription australia Settings‘, unaweza kwenda moja kwa moja kwenda ukurasa huo kwa kubofya hapa ->https://www.facebook.com/settings?tab=videos
 3. Bofya eneo la mwisho kulia limeandikwa ‘ where to order propecia online Auto-play Videos‘, chaguo Off kutoka kwenda orodha ya uchaguzi itakayoonekana ukibofya.
INAYOHUSIANA  Facebook katika ulimwengu wa mahaba

Kwenye Facebook App – Android

Kama unatumia huduma ya Facebook kupitia toleo la app ya Android basi fuatilia hatua hizi kuzima video kujicheza zenyewe ukiwa unatumia app ya Facebook.

 1. Bofya kwenye alama ya mistari mitatu iliyolala.
 2. Shuka chini na bofya eneo la App Settings
 3. Bofya ‘Video Auto-play
 4. Bofya ‘Off‘ kuzuia kabisa video kucheza zenyewe au bofya ‘Wi-fi only‘ ili kuruhusu video kucheza zenyewe pale tuu unapokuwa unatumia huduma ya intaneti kupitia mfumo wa WiFi.

Kwenye Facebook App – iOS (iPhone)

Kama unatumia huduma ya Facebook kupitia app katika simu za iPhone basi fuatilia hatua hizi kuzima video kujicheza zenyewe ukiwa unatumia app ya Facebook.

 1. Bofya kwenye alama ya mistari mitatu iliyolala,
 2. Shuka (scroll) chini na bofya Settings
 3. Bofya Account Settings
 4. Bofya Videos and Photos
 5. Bofya ‘Auto-play’
 6. Bofya ‘Never Auto-play Videos‘ na basi utakuwa umekwamisha kabisa video kujicheza zenyewe ukiwa unatumia huduma ya Facebook, ila kama bado utataka hali hiyo iendelee pale tu unapokuwa kwenye huduma ya intaneti ya WiFi basi chagua ‘WiFi Connections Only’.
INAYOHUSIANA  Instagram yazindua IGTV. IGTV ni nini?

Kwente Facebook App – iOS (iPad)

iPhone na iPad zinatofautiana mambo kadhaa kwenye mipangilio yake (settings) na ata kwenye app ya Facebook hali ni ile ile. Kujua jinsi ya kuzuia video kujicheza zenyewe ukiwa unatumia app ya Facebook fuata hatua hizi;

 1. Bofya kwenye alama ya mistari mitatu iliyolala ukiwa ndani ya app ya Facebook
 2. Shuka chini na bofya Account Settings
 3. Bofya Videos and Photos
 4. Bofya Auto-play
 5. Bofya Never Auto-play Videos basi utakuwa umekwamisha kabisa video za Facebook kujicheza zenyewe ukiwa unatumia app ya Facebook, ila kama bado utataka hali hiyo iendelee pale tu unapokuwa kwenye huduma ya intaneti ya WiFi basi chagua ‘WiFi Connections Only‘.
INAYOHUSIANA  Facebook ina mbinu ya kuwa karibu na mkufunzi

Je umekuwa ukichukizwa au kufurahia huduma ya video za Facebook na kujiplay zenyewe yaani ‘autoplay’? 🙂

Tuambie kupitia eneo la comment, kwa makala mengine ya ‘Maujanja’ yanayokufundisha jinsi ya kufanya mambo mbalimbali tembelea eneo la Maujanja katika mtandao wako wa TeknoKona

Picha na The Forbes na Google.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply