Kaa Tayari,Baada Ya Nokia 9 Sasa Nokia 8 Ipo Njiani!

0
Sambaza

Nokia ni simu ambazo zilipata umaarufu sana hapo mwanzo na kuwa ndio namba moja kama simu zinazopendwa sana duniani.

Licha ya Nokia kuuza sana. simu hizi zilipotea baada ya kampuni kuuza leseni yake kwa kampuni ya Microsoft. Ukiachana na hayo, tunajua kabisa kuwa kwa sasa kampuni imerudi na imekuja na simu nyingi ambazo zinaendeshwa na programu endeshaji ya Android

Inayosemekana Kuwa Nokia 8

Matoleo mengi yameshatoka na kwa sasa taarifa zilizopo ni kwamba toleo la Nokia 8 lipo njiani. Inategemewa kuwa Nokia 8 iwe ni toleo bora zaidi katika simu za Nokia ambazo tayari zimeshatoka.

SOMA PIA:  OnePlus 5; Ijue Siku Ya Uzinduzi Na Uwezo Wake!

Nokia kwa hali na mali inaonekana dhahiri kuwa wanapambana ili kuhakikisha kuwa wanakaa katika moja ya nafasi tano za juu katika watengenezaji wa simu.

HDM Global ambao ndio wamiliki na watengenezaji wa simu za Nokia wamesema kuwa wataitisha tamasha kubwa mnamo Agosti 16, 2017 ambapo ndio Nokia 8 itakapo zinduliwa.

Kwa sasa hakuna chochote cha ziada kinachojulikana juu ya simu hii isipokuwa tarehe hiyo tuu. Mambo mengi yataanza kufahamika ifikapo tarehe hiyo au kama taarifa zingine zitokee siku za usoni.

SOMA PIA:  Samsung Galaxy X kuwa simu ya kwanza yenye kioo chenye kujikunja na kujikunjua? #Uchambuzi

Nokia 3

Ningependa kusikia kutoka kwako, je ungependa kutumia simu ya nokia tena? niandikie hapo chini sehemu ya comment.

Kumbuku Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwa Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com