Satelaiti ndogo zaidi yaundwa nchini India - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Satelaiti ndogo zaidi yaundwa nchini India

0
Sambaza

Teknolojia ni suala linalokuwa kila siku na kama ukitaka kuwa mtaalamu katika masuala ya teknolojia huna budi kuwa mtu wa kupenda kujua kuhusu mambo mapya yanayotokea kila leo katika suala zima la teknolojia.

go to link

enter site Satelaiti ambazo zinasaidia katika mambo mbalimbali huko angani sasa mapya yametokea katika uundaji wa satelaiti. Kijana mmoja nchini India ameunda kile kinachotajwa kuwa setilaiti ndogo zaidi ambayo itawekwa kwenye mzingo wa dunia katika kituo cha shirika la safari za anga za juu la Marekani NASA mwezi Juni.

KijanaRifath Shaarook kutoka India akionesha ubunifu wake

Kifaa hicho kilichotengenezwa na kijana wa miaka 18, Rifath Shaarook cha uzito wa gramu 64, kilichaguliwa kama mshindi wa shindano lililodhaminiwa na NASA.

KalamSat

Satelaiti ndogo yenye lengo la kuonesha uwezo wa chapa (printer) ya 3D katika utengenezaji wa vitu vya aina mbalimbali.

http://alaptopshoppe.com/wp-content/uploads/fvm/cache/footer-d20f6795-1508548687.min.js Soma pia: India katika masuala ya anga

Satelaiti hiyo ilichaguliwa kutoka shindano kwa jina Cubes in Space, lililoandaliwa na NASA pamoja na kampuni ya elimu ya Idoodle. Setilaiti hiyo itasafiri kwa muda wa dakika 12 katika mazingira sawa na ya angani.

Satellite hiyo imepewa jina KalamSat, baada ya jina la rais wa zamani wa India Abdul Kalam, ambaye ni mwanzishi wa miradi ya anga za juu ya nchi hiyo.

Chanzo: BBC

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Sababu 5 kwanini ndege inapata ajali
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.