Kama vile Google na Project Ara: Acer waja na Kompyuta za Muunganisho

1

Sambaza

Tayari kampuni ya Google ipo katika utafiti na tayari ishatengeneza mifano ya simu ambazo utakuwa unanunua vipande (parts) na kuunganisha. Yaani hakutakuwa na mauzo ya simu nzima bali utakuwa una’upgrade kwa kununua na kupachika kifaa husika. Na sasa Acer wamekuja na mfumo huo huo na inaonekana muda si mrefu watakuwa ndio wa kwanza kabisa kutengeneza na kuuza kompyuta za teknolojia hii.

Uzuri wa teknolojia hizi ni kwamba tegemea kuweza kununua na kuuza vipisi (parts) unazobadilisha kwa urahisi kwa wengine kwani lengo kuu ni kuhakikisha vifaa hivyo vitaweza kuingiliana kwa urahisi.

Kipande cha kompyuta kuu, yaani CPU. Juu yake mtu anauhuru wa kuunganisha vipande vingine

Kipande cha kompyuta kuu, yaani CPU. Juu yake mtu anauhuru wa kuunganisha vipande vingine

click Tunamaanisha nini hasa tunaposema ununua vipande na unaunganisha?

INAYOHUSIANA  Terabyte sio mwisho kwa ukubwa wa memori

Mwanza kabisa utanunua kompyuta hii kiuzima wake ikiwa imeunganisha na sehemu (parts) zote muhimu. Yaani kutakuwa na kipande cha CPU, cha chaji, graphic card, diski (Hard disk), na kipisi cha masuala ya sauti.

Wengi wanategemea teknolojia ya namna hii kutumika kwenye simu janja na kompyuta kutashusha gharama na ulazima wa kutumia pesa nyingi kununua kifaa chenye teknolojia ya kisasa zaidi. Mara nyingi watu wanajikuta wakitumia pesa nyingi kununua simu mpya kisa tuu ya maboresho machache katika simu hizo, kama kungekuwa na uwezo wa kununua na kupachika bila ufundi wowote kitu hicho kipya basi wengi wangeweza kuokoa pesa nyingi sana.

Simu ya Project Ara kutoka Google

http://hazstat.com/12-512/ Simu ya Project Ara kutoka Google – Simu kutoka Google kupitia mfumo wa Project Ara, ni vipande mbalimbali ambayo unaviunganisha na unapata simu nzima. Utaweza kununua ‘parts’ za kuboresha zaidi kama vile ujazo, kioo, na mengine mengi

Acer wanaita vipande hivyo vinavyotumika kujenga kompyuta yako ‘Blocks’, yaani matofali. Na zitatambulika kama Acer Revo.

Acer wamesema muda wowote hivi karibuni wataanza kuuza kompyuta za teknolojia hii na hivyo watu wakae tayari kupata uhuru huu wa kipekee wa kuweza kufanya maboresho ya kompyuta zao kirahisi bila kununua kipya kila mwaka.

Kompyuta iliyokamilika, ikiwa imeunganishwa na CPU, Graphic card, spika, diski na chaja

buy doxycycline monohydrate Kompyuta iliyokamilika, ikiwa imeunganishwa na CPU, Graphic card, spika, diski na chaja

Mradi wa Google wa kutengeneza simu zinazofuata teknolojia hii unafahamika kwa jina la Project Ara na wanyewe Google wamesema simu hizo zitegemewe kuingia sokoni kuanzia mwaka 2016.

INAYOHUSIANA  Mbwembwe zinazokuja kwenye Windows 10

Uzuri wa teknolojia hizi ni kwamba tegemea kuweza kununua na kuuza vipisi (parts) unazobadilisha kwa urahisi kwa wengine kwani lengo kuu ni kuhakikisha vifaa hivyo vitaweza kuingiliana kwa urahisi.

Kompyuta hizo kadhaa zikiwa mezani. Acer Revo

Kompyuta hizo kadhaa zikiwa mezani. Acer Revo

Je, una maoni gani juu ya teknolojia hii ya muunganisho wa parts za kompyuta au simu bila ulazima wa kununua kifaa kizima kila toleo jipya likitoka? Tungependa kusikia kutoka kwako.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

1 Comment

  1. Pingback: Project Ara: Simu za Kuchomeka 'parts' kuletwa na Google

Leave A Reply