Kamera ya Megapixel 23, Kioo cha 4K: Ifahamu SONY XPERIA Z5 PREMIUM - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Kamera ya Megapixel 23, Kioo cha 4K: Ifahamu SONY XPERIA Z5 PREMIUM

1
Sambaza

Sony wamezindua toleo jipya la mtiririko wa simu za Xpreria itakayojulikana kama Sony Xperia Z5 katika maonesho ya kimataifa ya kiteknolojia yaliyofanyika Berlin, Ujerumani.

see

Simu hiyo itakayopatikana katika matoleo matatu kila moja ikiwa na kamera yenye uwezo wa Megapixeli 23 inayoongezewa nguvu na sense thabiti ya Sony, imeongezewa uwezo wa kupiga picha kwa kasi, pamoja na uwezo wa kupiga picha katika mazingira yenye mwanga hafifu.

buy fluoxetine 40 mg Simu kubwa zaidi katika matoleo ya Sony Xperia Z5, itajulikana kama Xperia Z5 Premium, na itakuwa na ukubwa wa nchi 5.5. Inakuja na kioo cha ‘resolution’ ya pixels 3,840 x 2,160, hichi ni kiwango kikubwa zaidi cha pixels katika simu janja kuliko simu nyingine nyingi. Hii inakipa kioo chake wastani wa pixel 806 kwa kila inchi wakati kioo cha simu ya iPhone 6 kina wastani wa pixels 326 kwa kila inchi, hii ni tofauti kubwa sana.

INAYOHUSIANA  iPhone mpya yenye laini mbili kuuzwa Uchina tu!

Mwanzo, simu za Sony zilikua na uwezo wa kurekodi video zenye pixeli 4K, lakini hazikuwa na kioo chenye uwezo wa kucheza video zenye ubora huo wa pixeli 4k.04sony-xperia-z5-compact-premium-3

Xperia Z5 sasa zinakuja na sensor maalum za kurekodi alama za vidole, kama zile za simu za iPhone 5S na iPhone 6.xperia_z5_press_02

Itakuwa na processor inayojulikana kama Qualcomm Snapdragon 810 yenye Octa-core CPU pamoja na uwezo wa intaneti wa 4G. Itakuja na toleo la Android la 5.1.1. Imebeba RAM ya GB 3, pamoja na diski uhifadhi (storage) wa GB 32.

Sony wanasema, upekee wa simu hii ni pamoja na Betri yake ya ndani yenye ukubwa wa 3430 mAh, itakayokuwa na uwezo wa kudumu kwa karibia siku mbili mfululizo.

INAYOHUSIANA  Google Calendar yaongezewa vipengele vizuri sana

Simu hii yenye ubora wa hali ya juu kabisa itauzika kwa dola 955 za Kimarekani, hii ni takribani Tsh Milioni 2 za Kitanzania.

Sifa kubwa kwa ufupi;

  • Kioo cha ubora wa hali ya juu (4K display)
  • ‘Fingerprint sensor’
  • Kamera ya ubora wa juu
  • Ubunifu wa kiwango cha juu

Ubaya;

  • Bei ghari, kutoa milioni mbili kwa ajili ya simu janja si jambo la kawaida. Unatakiwa uwe nazo kweli kweli
  • Kiwango cha betri kipo juu ila kutokana na uwezo mkubwa wa simu hiyo chaji inaweza isikae muda mrefu sana

Je, ulikuwa unapanga kunuua simu janja ya kiwango cha juu hivi karibuni? Basi hautakuwa umefanya makosa kujipanga na kuifikiria Sony Xperia Z5 Premium.

Facebook Comments
[review position="bottom"]
Sambaza
Share.

About Author

1 Comment

  1. Pingback: Sony watambulisha simu ya Xperia Z5 ya rangi ya Waridi

Leave A Reply