Hii ndio kampuni inayoongoza kwa mauzo ya Kompyuta duniani (Robo ya pili, 2017)

0
Sambaza

Kampuni ya Hewlett-Packard maarufu kama HP kwa mara nyingine tena imeendelea kuongoza katika ufalme wa soko la Kompyuta duniani.

Makampuni mawili ya utafiti wa soko la teknolojia, IDC na Gartner wote wanakubaliana kwamba HP kwa sasa ndio inashikilia soko la kompyuta duniani.

Kampuni ya utafiti ya Gartner ilisema Lenovo imeongoza kwa mauzo katika robo ya pili na kwa mujibu wa IDC robo ya kwanza iliongozwa na HP.

Kampuni ya HP yenye makao makuu yake California, nchini Marekani kwa mujibu wa utafiti uliotolewa na Gartner mauzo yake yamekuwa yakipanda mwaka baada ya mwaka katika uuzaji wa kompyuta zake.

SOMA PIA:  Kompyuta milioni 600 zinatumia toleo la Windows 10

Uongozi wa HP umekuwa mashakani kwa kukabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Lenovo. Utafiti huu unasema kufikia mwisho wa mwaka kunaweza kutokea mabadiliko ya kampuni yoyote kati HP na Lenovo kuongoza.

Hata hivyo kampuni ya Gartner imesema jambo la kutisha ni kwamba mauzo ya kompyuta yameendelea kushuka mwaka hadi mwaka ambapo mauzo ya robo ya kwanza kwa mwaka huu duniani kote ziliuzwa kompyuta milioni 61.1.

Kampuni hiyo ya utafiti ya Gartener imesema kushuka kwa soko la uuzaji kompyuta kumesababishwa na uwepo wa nguvu wa Simu janja (Smartphone) na Tablets.

mauzo ya Kompyuta duniani

Mauzo ya Kompyuta duniani: 

Na pia kumbuka ya kwamba ni kawaida mtu kutumia kompyuta ile ile kwa miaka mingi zaidi bila uhitaji wa kubadilisha wakati kwenye eneo la simu wengi wao hubadilisha mara kwa mara.

SOMA PIA:  Wadukuzi 10 hatari zaidi wa kompyuta duniani!

Vipi kwako, ni kompyuta/laptop za kampuni gani unazikubali zaidi kwa ubora wake?

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com