Kampuni ya utengenezaji magari ya Volvo kufungua kiwanda nchini Kenya - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Kampuni ya utengenezaji magari ya Volvo kufungua kiwanda nchini Kenya

0
Sambaza

Moja ya kampuni nguli kabisa katika utengenezaji magari mbalimbali – Volvo kufungua kiwanda nchini Kenya.

Kampuni hiyo imepanga kuwekeza Shilingi bilioni 2.5 za Kenya ambazo ni takribani Sh. Bilioni 52 – 54 za Kitanzania na hivyo kufanikisha utengenezaji wa haraka wa kiwanda hicho kwa ajili ya utambulisho rasmi kufikia mwezi Machi mwaka 2018.

volvo kufungua kiwanda nchini Kenya

http://blog.hearthstonegrill.com/wp-json/oembed/1.0// Volvo kufungua kiwanda nchini Kenya: Kwenye utambulisho wa makubaliono, Volvo walisema wamechagua mji Mombasa kuwa sehemu ambayo kiwanda hicho kitajengwa

Kiwanda hichi kitakuwa ni cha tatu barani Afrika kwa kampuni ya Volvo, tayari wana viwanda vingine nchini Afrika Kusini na Morocco. Wanategemea katika kipindi cha mwaka mmoja waweze kuzalisha magari 500, baadae wanataka kukuza uzalishaji huu na kufikia magari 2000 kwa mwaka.
Kiwanda hicho kitatengenezwa kwa ubia na kampuni nyingine ya Kenya ambayo imekuwa ni muagizaji pekee wa magari ya Volvo kwa soko la Afrika Mashariki, ya NECST Motors.

follow Viwanda hutengeneza ajira nyingi, moja kwa moja na zile zisizo za moja kwa moja kama vile katika sekta ya vyakula kwa wafanyakazi na nyingine nyingi

Ajira takribani 300 za moja kwa moja zinategemewa kutengenezwa na kiwanda hicho.

Lengo kuu kwa Volvo ni kuhakikisha wanazidi kukua na kushikilia vizuri soko la magari la Afrika Mashariki. Wanafanikio ya kushikiria soko la magari aina ya maroli/mabasi kwa asilimia 20 nchini Morocco na asilimia 18 nchini Afrika Kusini na sasa lengo lao ni kufikia asilimia 20 pia Afrika Mashariki.
Volvo ni kiwanda cha nne cha utengenezaji magari nchini Kenya. Kiwanda cha Volkswagen kiliacha utengenezaji takribani miaka 40 iliyopita ila nacho kimeanza utengenezaji magari nchini humo tena. Pia tayari makampuni mengine kama vile Peugeot, Iveco na Ashok Leyland wameshatangaza nia za kufungua viwanda nchini humo pia.

Je una mtazamo gani juu ya mafanikio haya kwa nchi jirani? Endelea kutembelea Teknokona kwa habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Namba za madereva wa Uber kutoonekana Kenya
Share.

About Author

click Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.