fbpx

Kodi ya mitandao: Kampuni za simu kuzuia VPN nchini Uganda

0

Sambaza

Karibuni watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini Uganda wanaoingia kupitia programu tumishi za VPN ili kuepuka kulipa kodi kwenye huduma za Over-the-Top (OTT) hawatakuwa na uwezo huo baada ya serikali ya Uganda kuzitaka kampuni za mawasiliano kuzuia programu hizo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa tume ya mawasiliano ya Uganda, Bw. Gofrey Mutabazi amezitaka kampuni za simu kuanza kuzuia polepole programu tumishi za VPN ili wale wanaojaribu kukwepa kodi wasiweze kufungua mitandao ya kijamii inayotakiwa kulipiwa kodi kabla ya kuitumia.

Pamoja na mpango wa kuzuia matumizi ya VPN, Mutabazi amesema kuwa programu za VPN ni nyingi hivyo itakuwa ngumu kuzuia zote na watalazimika kuzifunga baadhi.

Kampuni za simu kuzuia VPN

Mkurugenzi wa tume ya mawasiliano ya Uganda Gofrey Mutabazi aamewataka Waganda kulipa kodi kwani hayo ndio maamuzi ya kisheria yaliyopitishwa na serikali na wala sio mamlaka yake.

Kodi kwa mitandao ya kijamii imeanza kutumika nchini Uganda kwenye mwaka mpya wa fedha 2018/2019 (julai Mosi). http://maplegrovesprings.com/wp-json/oembed/1.0/embed?url=http://maplegrovesprings.com/amenities/yurts/north-yurt/ Ambapo mwananchi anatakiwa kulipa shilingi za Uganda 200 kwa siku au 1,400 kwa wiki/6,060 kwa mwezi.

Kampuni za simu kuzuia VPN

Ambayo itatokea kutokana na kuwekwa kodi kwenye matumizi ya mitandao ya kijamii.

Zoezi hilo limeleta usumbufu kwa wananchi wengi nchini Uganda kiasi cha kuwafanya wengine kuanza kutumia programu tumishi za VPN ili kuperuzi mitandao ya kijamii bila ya kulipa kodi.

INAYOHUSIANA  Hizi hapa namba zinazotumika kwa utapeli wa mtandaoni

http://grandavenueweddingofficiants.com/fees-and-services Moja ya kazi za VPN ni kumuonesha muhusika kwenye eneo ambalo sio halisi. Mfano mtumiaji yupo Uganda lakini kwa kutumia programu ya VPN anaweza kuonekana yupo Tanzania/Kenya au nchi yoyote atakayoamua aonekane.

Kampuni za simu kuzuia VPN

Namna VPN inavyofanya kazi.

Kwa kufanya hivyo ataweza kufungua mitandao ya kijamii iliyofungiwa Uganda kwa kuwa VPN inamuonesha kama mkazi asiyeishi Uganda.  Kwa muda wa siku tatu watumiaji wa Intaneti nchini Uganda wamepakuwa programu za VPN zaidi ya mara milioni 1.5.

Kwa mujibu wa utafiti wa kitaifa wa mamlaka ya habari na taknolojia Uganda (NITA-U), inakadiriwa kwamba zaidi ya asilimia 70 ya raia nchini Uganda wana simu za mkononi.

Vilevile, 41% ya raia nchini humo wanatumia intaneti kufikia mitandao ya kijamii kama Facebook na Twitter iliyo maarufu zaidi nchini humo.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.