Sambaza

Kama wewe ni mpenzi na mtumiaji wa mtandao wa kijamii wa Instagram basi kampuni hiyo imejipanga kukuboreshea  namna ya upakiaji wa picha kwenye mtandao huo kwa kukupa uwezo wa kupakia picha kubwa na zenye ubora mkubwa zaidi.

Muda si mrefu utaweza kupakia(upload) picha zenye ukubwa wa hadi 1080×1080 pi, hii ni baada ya kupokea malamiko ya muda mrefu kutoka kwa watumiaji wa app hiyo ambayo imekuwa inakuruhusu kupakia picha zenye ukubwa wa 640×640 pi tokea ilipokua imeanzishwa.

picha za instagram kua kubwa

picha za instagram kua kubwa

Taarifa hizo zimetolewa na mzungumzaji wa kampuni hiyo alipokua anaongea na mtandao wa kiteknolojia wa The Verge. Mzunguzaji huyo amesema tayari wameanza kujaribisha huduma hio kwenye baadhi simu janja za mkononi zinazotumia mfumo wa uendeshaji wa Android na iOS na pia aliongeza kwa kusema wanatambua jinsi teknolojia ya utengezaji  simu janja ilivyokua na kufikia uwezo wa kubeba kamera zenye uwezo mkubwa wa kutoa picha kubwa na bora zaidi.

SOMA PIA:  Twitter: Watu wanatwiti zaidi, ila twiti zao si ndefu sana

Kama huduma hii ikifanikiwa vizuri wataweza kuondoa kero iliyokua muda mrefu kwa watumiaji ambao walikua wanalazimika kukata na pengine kuharibu picha zao ili kuzipakia kwenye mtandao huo.
.

Endelea kutembelea mtandao wako namba moja kwa habari na maujanja ya kiteknolojia, kumbuka unaweza ungana nasi pia kupitia Instagram – www.instagram.com/teknokona

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com