Kampuni ya Kaspersky Lab imeshinda zabuni ya kutoa huduma za usalama wa kimtandao kwa vikosi vya jeshi la nchi ya Brazil.
Baada ya ushindaji mkali wa mchakato wa kutafuta kampuni stahiki ya kufanya kazi hiyo Kaspersky Lab ilipata zabuni hiyo kwa mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya dola milioni 2.6.
Dola Milioni 1.4 itakuwa kwa ajili jeshi la Anga pekee, Dola 735,000 kwa Ulinzi wa kimtandao na Dola 512,000 kwa ajili ya jeshi la majini. (Dola moja ya Marekani ni takribani Tsh 2,250/= kwa sasa)
Kaspersky Lab haikutoa maelezo ya programu gani maalum ambazo Vikosi vya Jeshi la Brazili zitatumia au wakati wa kuanza kazi hiyo.
Lakini tangazo rasmi la kampuni hiyo linasema kwamba kompyuta 120,000 zitakuwa na programu mpya ya Antvirus ya Kaspersky.