Shirika la Ndege la Kenya Airways limetangazwa kuwa ndio shirika bora zaidi katika uchukuzi wa ndege nchini Kenya kwa matumizi ya teknolojia.
Kenya Airways ilitwaa katika tuzo za Digital Inclusion Awards, 2017 zilizotolewa Jijini Nairobi mwishoni mwa juma. Tuzo hizo hutolewa kwa kampuni ambazo zinatumia teknolojia zaidi katika operesheni zake kwa lengo la kuboresha huduma kwa wateja.

Kenya Airways yashinda tuzo ya matumizi ya teknolojia 2017
Hii ni kutokana na kuwa kampuni hiyo imeimarisha majukwaa yake ya kielektroniki ya kuwahudumia wateja wake na kuwasiliana nao.
Wateja wake wanaweza kulipia safari zao moja kwa moja kwa kutumia huduma ya PesaLink au kwa njia ya simu. Kampuni zingine zilizoteuliwa kwa tuzo hiyo ni Fly 540, Air Kenya, Jambo Jet na Safari link Aviation.
Facebook Comments