fbpx

Kicharazio cha kwenye MacBook na MacBook Pro kubadilishwa bila malipo

1
Sambaza

Moja ya toleo la kompyuta mpakato kutoka Apple imepata malalamiko mengi kwa waliozinunua na hivyo kuwafanya Apple kufikiria kuwabadilishia kile ambacho kina matatizo bila ya wao kulipia (BURE).

Tatizo hilo lipo kwenye kicharazio cha kwenye MacBook/MacBook Pro na tatizo lililoelezwa ni where can i buy prednisolone tablets for dogs in the uk herufi kutotokea pale zinapobonyezwa au herufi kujirudiarudia pale inapobonyezwa.

Kicharazio cha kwenye MacBook/MacBook Pro ni kile kilichoundwa katika muudo wa herufi “V” au maarufu kama kipepeo kama ilivyozoeleka na wengi tofauti na matoleo mengine yaliyopita ambapo kwenye kicharazio zinatumia teknolojia ya muundo wa herufi “X”.

Kicharazio cha kwenye MacBook

Kicharazio cha kwenye MacBook kimeonekana kuleta shida pale vumbi/uchafu mwingine unapoingia jambo ambalo ni tofauti kwa vicharazio vilivyotengenezwa kufanya kazi katika muundo wa herufi “X”.

Kwa taarifa rasmi iliyotolewa na Apple imekiri tatizo hilo na kuamua mteja kwenda kwa wakala aliyeidhinishwa na wenyewe (Apple) ili kuweza kubadilishiwa kicharazio cha kwenye kompyuta yake (MacBook au MacBook Pro 2015).

Ambacho pengine hukifahamu….

Kompyuta MacBook ya inchi 12 (2015), 13 na 15 (2016) zipo kwenye mpango unaogharamiwa na Apple wa kuzifanyia matengenezo kompyuta ambazo zilizotajwa na zina miaka minne au chini ya hapo (2015-2018) tangu kununuliwa kwake.

Apple wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanalegeza misimamo yao ili kulinda heshima yao na hata kuvutia watu wengine. Hii itakumbukwa kwama ulivyotangaza kubadilisha baadhi ya betri kwenye iPhone mwaka mmoja uliopita.

Vyanzo: The Guardian, The Star Online

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Kompyuta inaanza kuwa nzito kiufanisi.. Sababu ni nini?
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|