Kigogo wa Samsung aliyehukumiwa jela miaka 5 aachiwa huru

0
Sambaza

Mrithi na tajiri wa Kampuni ya Simu za Samsung, Lee Jae-yong ameachiwa huru na mahakama ya Korea Kusini baada ya mahakama hiyo kumuondolea adhabu ya miaka mitano jela kufuatia mashtaka ya kumuhonga aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Park Geun-hye.

Katika mahakama ya rufani, mahakama hiyo ilikubaliana na baadhi ya sehemu ya mashtaka lakini ilitumia busara kumwachia kutokana na nafasi yake ya utendaji. Hata hivyo, mahakama ya Juu ya Korea Kusini inatarajiwa kukatia rufaa uamuzi huo.

Kigogo wa Samsung aliyehukumuiwa jela miaka 5 aachiwa huru

Kigogo wa Samsung aliyehukumuiwa jela miaka 5 aachiwa huru

Bw Lee alikuwa ameshtakiwa kuhusika katika rushwa katika kashfa ambayo pia ilichangia kuondolewa madarakani kwa rais wa zamani wa Korea Kusini.

SOMA PIA:  Mambo 8 ambayo si rahisi kujua kwenye simu za Samsung Galaxy

Bw Lee, ambaye pia hufahamika kama Jay Y Lee na amekuwa ndiye kiongozi wa kampuni hiyo kubwa zaidi ya kuunda simu duniani, amekuwa kizuizini tangu Februari akikabiliwa na tuhuma kadha za rushwa.

Lee, 49, pia alituhumiwa kutoa mchango wa hisani wa won 41bn ($36m; £29m)  zilizosimamiwa na rafiki wa karibu wa rais aliyeondolewa madarakani Park Geun-hye, ndipo apendelewe kisiasa.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com