Kijana mmoja anasa kwenye choo akijaribu kuokoa simu janja

0
Sambaza

Kijana mmoja nchini Norway alijikuta akiwa amenasa na kushindwa kutoka kwenye choo baada ya kuingia ili kuchukua simu iliyokuwa imedondokea chooni.

anasa kwenye choo

Anasa kwenye choo: Kushoto, vinaonekana vidole tuu, akiwa amenea, Kulia, Kijana huyo akionesha sehemu alizoumia alipokuwa anajaribu kutoka

Rafiki yake kijana huyo inasemekana alidondosha simu yake kwenye shimo la choo wakati anakojoa. Ni choo cha kadamnasi (public toilet), kijana huyo akajitolea kwenda kuitoa simu hiyo.

Inasemekana kijana huyo aliingia kwenye choo cha mfumo wa tenki chini ambacho huwa kinatolewa uchafu mara kadhaa tuu kwa mwaka. 

Inasemekana kwa akili yake alifikiri kitakuwa hakina uchafu mwingi kwa wakati huo ila alipoingia ndani akajikuta amesimama kwenye uchafu uliomfikia hadi maeneo ya mapajani. Alitapika, akashindwa kuipata simu na baada ya hapo ndio alianza kuangaika kutoka.

Muonekano wa choo hicho baada ya kukatwa ili kuweza kumtoa kijana aliyenasa

Alipojaribu kupanda tena kupitia tundu la choo alilotumia alinasa, na hivyo kushindwa kutoka hadi pale watu jiji walipokuja kumtoa.

Mara moja baada ya kutolewa alipelekwa hospitali alipooga na kuchomwa sindano za kuzuia maambukizi.

Haijaweza kujulikana ni simu ya aina gani alikuwa anaitafuta ila kwa haraka haraka unafikiri ni simu gani inaweza mpa mtu ujasiri wa kuingia kwenye shimo la choo kuisaka?

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
SOMA PIA:  Nokia matatani kwa wizi wa teknolojia!
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com