Pombe inayotokana na mkojo wa binadamu! #Teknolojia

0
Sambaza

Wengi wanaamini kuwa mkojo ni dawa lakini fikiria sasa mkojo utumike kutengenezea pombe, utakuwa tayari kuinywa pombe hiyo?

Katika hali ya kuwa na pombe zilizotokana na vimea mbalimbali ni dhahiri kuwa mkojo wa binadamu umekuwa mstari wa mbele kutumiwa katika utengenezaji wa pombe na nchini Denmark Kiwanda kimoja cha pombe kimetengeneza bia mpya kwa kutumia shayiri ambayo imekuzwa kwa kutumia lita 50,000 za mkojo.

Mkojo huo ulikusanywa kutoka tamasha ya Roskilde ambayo ndiyo hafla kubwa zaidi ya muziki Ulaya kaskazini miaka miwili iliyopita.

Pombe inayotokana na mkojo

Pombe ijulikanayo kama Pisner ikiwa katika mchakato wa utengenezwaji wake.

Pombe hiyo imeonekana kuvutia watu mbalimbali na mmja ya wanywaji wa pombe hiyo inayotokana na mkojo alithubiti kusema kama ingekuwa na ladha ya mkojo ningeachana nayo, lakini hata huwezi ukahisi.

SOMA PIA:  Teknolojia ya FaceID kuruhusu uso mmoja tu kusajiliwa

Soma pia: Mashine inayotumia umeme wa Jua inayogeuza mkojo kuwa pombe

Ingawa pombe hiyo inatengenezwa lakini baraza la chakula la nchini  Denmark limetoa ushauri wa kutumiwa kwa mkojo kama mbolea ya kurutubisha shayiri ambayo baadaye inatumiwa kutengeneza pombe.

Wakati bia hiyo inaanza kutengenezwa watu walidhani kampuni inayotengeeneza bia hiyo walikuwa wanaweka mkojo moja kwa moja baada ya bia hiyo kutengenezwa lakini bada ya muda walikuja kuelewa si vile walivyokwa wanavyofikiria.

SOMA PIA:  Uwepo wa simu janja kwa miaka 25 #Ripoti

Kampuni ya Norrebro Bryghus inayomiliki kiwanda hicho hata hivyo imesema bia hiyo haitakuwa na masalio yoyote ya mkojo wa binadamu. Je, bia hiyo ikiletwa huku kwetu utakuwa tayari kwa kunywa?

Vyanzo: BBC, Reuters

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com