Kilimo cha siku hizi kimekuwa na changamoto za hapa na pale lakini kwa ambao wameshaweza kutumia fursa ya uwepo wa kilimo cha kisasa wamekuwa wakinufaika kutokana na kutumia teknolojia zaidi.
Tatizo la vijana kukimbilia mijini kutafuta kazi nyingine za kufanya na kuacha ardhi yenye rutuba vijijini limekuwa ni tatizo ambalo linasumbua nchi nyingi duniani. Kwa kikubwa teknolojia imeonekana kuwa msaidizi kwa vitu vingi na kwa hili pengine likawavutia wakulima:
Matumizi ya ndege zisizo na rubani (drones) zimekuwa zikitumiwa na wakulima wa mpunga nchini Japan. Kilimo hicho kinatumia ndege kumwaga dawa shambani kwa ajili ya kukinga dhidi ya magonjwa/wadudu waharibifu.
Kwanini matumizi ya ndege zisizo na rubani zimekuwa kivutio?
Wakulima wengi Japan wana umri wa miaka 67-68 kwa wastani na kutokana na ukweli kwamba nguvu za watu wenye umri huo zimepungua lakini ndege isiyokuwa na rubani inaweza kunyunyuzia dawa/mbolea shamba zima la mpunga kwa muda wa robo saa; iwapo uktumia rasilimali watu kufanya kazi hiyo ingechukua zaidi ya saa moja kumaliza kazi hiyo.
Ndege hizo zinaweza kuongozwa ka kutumia tabiti (iPad) na programu wezeshi ya ramani ambayo ni rahisi kuielewa na kuitumia hivyo anachohitaji mkulima ni kukaa sehemu na kuongoza kifaa hicho.
Bei yake sio rahisi….
Ndege hiyo kukamilika kwa ajili ya kazi za kilimo inagharimu $135,758|Tsh. 312,243,400. Ni fedha nyingi lakini kwa Japan makampuni mbalimbali yanatoa huduma hiyo (kilimo cha kutumia ndege isiyokuwa na rubani) lakini kw malipo fulani.