Kionjo: Apple Yamwaga Trilioni 4.8 kwa Dr. Dre

0
Sambaza
image

Dr Dre

Kampuni ya Apple Inc. imeripotiwa rasmi kuwa wamiliki wa kampuni ya ‘headphone’ ya Beats Electronics baada ya kutumia takribani dola bilioni tatu za kimarekani kuinunua kampuni hiyo iliyoanzishwa na prodyuza mkongwe wa miondoko ya hiphop, Dr. Dre  na mwenzake Jimmy Lorine wa Interscope records.

Kampuni hiyo ambayo pia inatoa huduma ya kusikiliza muziki mtandaoni imeifanya Apple kutumia hela nyingi zaidi ya manunuzi yote iliyowahi kufanya.
Katika dili hilo lililofanyika rasmi baada ya wiki kadhaa za hayawi hayawi, inasemekana Dr. Dre na Jimmy Lorine watabaki kwenye kampuni hiyo ‘iliyokuwa’ wakiwa waajiriwa wa kampuni ya Apple ingawa haijajulikana watakuwa na vyeo gani.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
SOMA PIA:  Apple yapunguza bei ya betri ya simu zake
Share.

About Author

Ninafuatilia teknolojia kila siku na ninapenda kutoa ujuzi wangu kuhusu teknolojia. Karibu tuzungumze kuhusu teknolojia hapa teknokona!

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com