fbpx

Youtube: Kipengele cha Dark Mode kwenye simu

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +

vodacom swahili

Sambaza

Kampuni ya Google imethibitisha kwamba kipengele cha mandhari ya Dark Mode kwa watumiaji wa YouTube kimeanza kupatikana kwa simu zenye kutumia mfumo endeshi wa Android.

Kipengele cha Dark Mode kilitangazwa kupatikana tangu mwezi Machi mwaka huu lakini kilikuwa kinapatikana kwa watumiaji wa simu za mfumo wa iOS. Kwa watumiaji wa kompyuta Dark Mode ilianza kupatikana tangu Mei 2017.

Kwa kawaida muonekano wa YouTube kwa muda wote umekuwa wa rangi Nyeupe (white background) lakini ujio wa Dark Mode mtumiaji atakuwa na chaguo aidha aweke Nyeupe au Nyeusi.

Kipengele cha Dark Mode

Namna ya kuweka mandhari ya Dark Mode kwenye YouTube yako ni kuingia Settings kisha General ambapo utaona Neno Dark Theme na utalichagua

Ikiwa kwenye YouTube ya kwenye simu yako hutaona kipengele cha Dark Theme, basi jaribu kupakua masasisho na bado hutaona kipengele hicho basi kuwa mvumilivu kwani utakuwa bado haujawezeshwa.

Utumiaji wa mfumo-Dark Mode unasaidia sana kwenye utunzaji wa chaji kwenye simu kutoisha mapema zaidi ukilinganisha unavyoperuzi Youtube ikiwa kwenye ule muonekano ambao unafahaika na wengi.

Mabadiliko haya yameanza kuwafikia watu wa nchi mbalimbali ambao wameonyesha ushahidi wa kupata kipnengele cha mandhari ya Dark Mode.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Redmi 7: Simu nzuri halafu kwa bei ya kawaida
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.