Kipengele cha ‘Smart Battery’ kwenye simu za Google Pixels

0
Sambaza

Simu janja ambazo kwa asilimia zote zimetengenezwa na Google ambazo tayari zimeshaingia sokoni zimeongezewa kipengele cha kufanya makadirio mazuri zaidi katika betri linavyoisha chaji kulingana na jinsi linavyotumika.

Katika kitu ambacho watengenezaji wanakumbana katika biashara ya utengenezaji wa simu janja na kujitahidi kuwa toleo lijalo/simu janja itakayofuata itakuwa bora au kuwa na uwezo zaidi ni upande wa betri husika kukaa na chaji kwa muda mrefu.

Kuna programu tumishi mbalimbali kwenye soko la Google na kupakua programu tumishi ambazo zinafanya kazi ya kutoa makadirio ya kiasi cha betri ambacho simu husika imetumia lakini matokeo yake yamekuwa tofauti na matarajio.

Battery Doctor-moja ya apps ambayo inaonyesha makadirio ya matumizi ya betri.

Kilichoboreshwa na Google kwenye simu za Pixels katika sasisho jipya.

Tangu simu za Google Pixels zinazinduliwa tayari zilikuwa na uwezo wa kuonyesha kiasi cha betri kilichotumika pamoja na makadirio ya muda gani simu hiyo/hizo zitakaa na chaji mpaka kuhitaji kuchajiwa tena lakini kwa mujimu wa Google kipengele hicho kilikuwa hakitoi takwimu sahihi.

Google imeboresha vilivyo kipengele cha kuonyesha kiasi ambacho betri imetumika kwa mfumo wa asilimia pamoja na kuonyesha makadirio ya muda ambayo simu za Google Pixels zitahitaji kuchajiwa kwa mara nyingine tena.

Smart battery-kipengele kipya kwenye simu za Google Pixels ambacho kimeboreshwa na kutoa makadirio kulingana na matumizi ya simu husika.

Google imesema makadirio ambayo kipengele cha Smart Battery (kabla ya maboresho) kilikuwa kikitoa kwenye simu hizo (Google Pixels), takwimu hizo zilitokana na kama katika saa moja mtu ametumia 10% ya betri na saa ya pili hivyo hivyo basi ilichukuliwa kuwa kila saa ni 10% tu ya kiwango cha betri ndio kunatumika.

Ni jambo la zuri kwa Google kuamua kuboresha kipengele cha takwimu za matumizi ya betri ili kutoa takwimu sahihi zitakazomuwezesha mtumiaji wa simu za Google Pixels kujua kwa usahihi kabisa muda ambao atahitaji kuchaji tena simu hiyo.

Vyanzo: Gadgets 360, 9to5Google, Android Authority

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
SOMA PIA:  Clips - App mpya kwa ajili ya iPhone na iPad
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com