Kipimo Janja cha Mimba Kinachotumia Bluetooth na App Kukupatia Taarifa! #Teknolojia - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Kipimo Janja cha Mimba Kinachotumia Bluetooth na App Kukupatia Taarifa! #Teknolojia

0
Sambaza

Wengi wameponda kuhusu ujio wa kipimo janja cha mimba kinachokupatia taarifa kama ni kweli unamimba au hapana kwa kutumia mawasiliano ya bluetooth na app unayoweka kwenye simu yako.

Wengi wanaona teknolojia ya muunganisho wa vifaa na huduma za kiintaneti, ‘internet of things’, inatumiwa hadi pasipo na ulazima ila pia wengine wanaona ni jambo zuri ila tungependa kusikia maoni yako baada ya kusoma zaidi.

Muonekano wa kipimo hicho

Muonekano wa kipimo hicho

Kipimo hichi kinafanyaje kazi?

Kama vile vipimo vingine vya mimba, mwanamke atakojoa na kulowanisha kifimbo spesheli na mkojo na kisha atapata matokeo.

Lakini utofauti ni kwamba katikati ya kukojelea kipimo hicho na kupata majibu kuna taarifa kadhaa zitakuwa zinatumwa kwenye app utakayokuwa umeipakua kwenye simu yako.

Je tunapoelekea tutakua na app kwa ajili ya kila jambo?

App hiyo itakuambia;

>Kama kiwango cha mkojo kilicholowanisha kifimbo hicho spesheli ni kiwango cha kutosha kuweza kupewa majibu
Pia utapata taarifa kama kifimbo hicho spesheli kinafanya kazi kwa usahihi

INAYOHUSIANA  Bios Cube: Majivu ya marehemu kutumika kukuza mmea

>Baada ya kulowanisha kipimo (kifimbo) hicho na mkojo kutakuwa na muda wa dakika tatu kabla ya kupewa majibu. Na katikati ya muda huo basi app hiyo itakuwa machaguzi matatu (options),

buy metformin 1000 mg Educate Me – Ukibofya hapo utapewa elimu mbalimbali zinazohusiana na uzazi
http://socialbard.com/black-tones-in-alexandria/ Entertain Me – Utaletewa video mbalimbali za kuburudisha wakati unasubiria matokeo yako
see url Calm Me – Hapa app hiyo itakuletea miziki ya kiutaratibu ya kukufanya utulie kidogo kama upo katika hali ya hofu

kipimo-mimba-2

Kitu kikubwa ni kukusaidia kutowaza sana suala la matokeo ya kipimo ulichofanya wakati unasubiria matokeo.

Kama nia yako uliyaichagua kwenye app ya kwamba unataka kupata mimba basi app hiyo itakupa hongera kama kipimo kitaonesha kuna mimba, na kama hakuna utapewa taarifa mbalimbali muhimu za kukusaidia.

INAYOHUSIANA  Fahamu Mambo Mapya Yanayokuja Kutoka WhatsApp

Je unafikiri utumiaji huu wa teknolojia ni muhimu? Au unaona tayari tuna apps nyingi na suala hili haliitaji msaada wa app kabisa? Tuambie tutafurahi kusikia kutoka kwako.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply