Kitu cha kujihadhari nacho kwenye WhatsApp - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Kitu cha kujihadhari nacho kwenye WhatsApp

0
Sambaza

Katika mawasiliano ya kila siku na kwa walio wenye simu janja kuwasiliana kupitia WhatsApp ni kitu cha kawaida sana kuliko hata kutumia njia ya kutuma ujumbe mfupi wa maneno kama ilivyokuwa huko nyuma kabla ya ujio wa programu tumishi maarufu sana duniani.

go to site

Kwenye WhatsApp imekumbwa na kirusi kibaya sana ambacho kinaweza kusababisha usiweze tena kutumia programu hiyo yenye watumiaji wengi duniani au hata kuharibu kabisa simu rununu hivyo kuifanya kutoweza kufanya kazi tena.

Tatizo hilo hinafahamika kama “Black dot” ambapo linaweza kuja katika namna mbili tofauti.

Swali ni je, kitu hicho kinaathiri vipi simu/programu husika? Namna ya kwanza inakuja katika http://nacflightnews.com/event/colonial-hills-christmas-tournament-varsity-only/ mfumo wa ujumbe wa maneno ikikupa onyo kuwa ukibonyeza nukta zilizowekwa chini simu yako itashindwa kufanya kazi kabisa au unapokea http://co-opmedianetwork.com/team/ ujumbe ambao unakuwa na maneno na alama ambazo hazieleweki na mara tu utakapobonyeza sehemu ya ujumbe husika yale yalijificha kwenye ujumbe yatatoka na kusababisha madhara makubwa kwenye simu/kifaa husika.

Kitu cha kujihadhari

Ujumbe ambao unaweza kupokea kutoka kwa mtu yeyote kwenye WhatsApp hivyo unapaswa kujihadhari nao kwa usalama wa kifaa chako.

Tatizo hilo limeelezwa linaweza kushambulia vifaa vinavyotumia programu endeshi ya iOS na kusababisha madhara yaleyale ambayo yanaweza kutokea kwenye simu zinazotumia mfumo endeshi wa Android.

Kitu cha kufanya ni ni kuwa makini na jumbe unazopokea kupitia WhatsApp ambazo hazieleweki au zinafana na kitu kilichoelezwa kwenye makala hii na mpaka wakati makala hii inaandaliwa Facebook (wamiliki wa WhatsApp) hawajatoa neno kuhusiana na tatizo hilo.

Vyanzo: Gadgets 360, Pixr8

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Instagram Lite Sasa Yaanza Kupatikana.
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.