Kivinjari cha Opera chaja na Uwezo wa Kuzuia Matangazo kwenye Tovuti (Mtandaoni)

0
Sambaza

Habari mbaya kwa mitandao inayotegemea mifumo ya matangazo ya kimtandao kuweza kujiendesha, vita dhidi ya matangazo ya mtandaoni yazidi kukua baada ya kivinjari maarufu ila kilichopoteza umaarufu kwenye kompyuta cha Opera kuja na uwezo wa kuzuia matangazo.

Kwenye vivinjari vingi uwezo huo huwa unaongezwa kupitia utumiaji wa plugin – viprogramu vidogo vinavyopatikana kwenye masoko ya apps za vivinjari.

opera matangazo zuia

Plugin maarufu ikiwa ni ya AdBlock Plus. Utumiaji wa plugin ingawa unafanya kazi vizuri tuu mara nyingi huwa unaitaji hatua nyingi kuweza kuuweka kwenye kivinjari chako na pia huwa zinaathiri utendaji kazi wa kasi wa kivinjari husika ilihali matangazo uzuiliwa.

Kupitia toleo jipya la kivinjari cha Opera kwa ajili ya kompyuta uwezo wa kuzuia matangazo umetengezwa ndani yake. Hii inasaidia kufanya jambo la kuzuia matangazo kuwa rahisi zaidi na lisilo athiri kasi ya kivinjari hicho. Afisa mmoja wa Opera alikaririwa akisema kuna tovuti zinazofunguka kwa zaidi ya asilimia 90 haraka zaidi pale matangazo yako yanapokuwa yamezuiwa ukilinganisha na yanapokuwepo.

opera

Kivinjari cha Opera chenye uwezo wa kuzuia matanganzo kinafanya kazi haraka zaidi ukilinganisha na vya Chrome na Firefox vikiwa na plugin ya AdBlock Plus

Data za utumiji vivinjari vya mwezi uliopita unaonesha kivinjari cha Opera kina miliki asilimia 2.07 za watumiaji wa intaneti katika mwezi huo. Hichi ni kiwango kidogo sana na hivyo wengi wanaona uamuzi huu unaweza pia ukawa umefikiwa kwa ajili ya kusaidia kuongeza watumiaji wa kivinjari hicho.

SOMA PIA:  PowerShake: Teknolojia ya kushare chaji kwa kutumia Wi-Fi #Maujanja

Kama kivinjari kama vile Firefox au Chrome kingefanya uamuzi huu basi ndio ungekuwa na athari ya haraka sana(kutokana na watumiaji wengi) kwa mitandao mingi zaidi inayotegemea mapato kupitia matangazo ya mtandaoni. Na inaonekana ni uamuzi mgumu kufanywa kwa Chrome kwani kivinjari hicho kinamilikiwa na kampuni ya Google, ambao wanategemea mapato makubwa kupitia mfumo wao wa matangazo ya mtandaoni.

Wakati plugin ya AdBlock Plus huwa inaruhusu baadhi ya matangazo kuruhusiwa kama si ya usumbufu zaidi wao Opera wanazuia matangazo ya aina zote. Ingawa utakapopakua toleo lao hili na kuanza kutumia matangazo yatakuwa yameruhusiwa kwenye tovuti zote unazotembelea, kivinjari hicho kitakuuliza kwenye tovuti husika kama unataka kuvuia matangazo, na ukikubali basi matangazo yote kwenye tovuti hiyo yatazuiwa kuonekana tena.

Matangazo yanazuiwa kwa tovuti husika...

Matangazo yanazuiwa kwa tovuti husika…

Je una mtazamo gani juu ya matangazo ya mtandaoni? Unaona wamefanya uamuzi mzuri au sio fresh?

Kama unaharaka ya kujaribu toleo hilo;

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com